MWALIMU WA KRISTADELFIANI
back

l. Nini maana ya neno au jina "Kristadelfiani"?

Jibu: Inamaanisha ndugu au jamaa wa Kristo. Ni jina la Kristo na ndugu ikiwa imeambatanishwa pamoja katika lugha ya Kiyunani.

2. Ndugu au jamaa wa Kristo ni nani?

Jibu: Ni yule anayetekeleza mapenzi yake Mungu.

Thibitisho: "Kwa maana ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu" (Mathayo 12:50). ''Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu" (Yohana 15:14-15).

3. Mapenzi ya Mungu tunayopaswa kutekeleza ni yapi?

Jibu: Tumwamini mwanawe Yesu Kristo na kutii amri zake.

Thibitisho: "Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye'' (Yohana 6:29). "Na hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina 1a Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri. Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye, naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa" (1 Yohana 3:23, 24).

4. Ni nani amewapa jina hili "Ndugu wa Kristo'' wale wanaotekeleza mapenzi yake Mungu?

Jibu: Ni Kristo mwenyewe aliyewapa.

Thibitisho: "Maana yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake; akisema, Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu; Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa "(Waebrania 2:11, 12). ''Kisha Yesu akawaambia, Msiogope; enendeni, mkawaambia ndugu zangu waende Galilaya, ndiko watakakoniona" (Mathayo 28:10). "Akawatazama wale walioketi wakimzunguka pande zote, akasema, Tazama, mama yangu na ndugu zangu" (Marko 3:34). "Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoini mwa ndugu wengi" (Warumi 8:29).

5. Kwa nini Ndugu wa Kristo wanaitwa Wakristadelfiani badala ya kuitwa tu Wakristo siku hizi zetu?

Jibu: Kwa sababu watu wengi wanaitwa wakristo wasiotii amri za Kristo. Ukristo uliopo umekuwa mkondo wa imani ya hadithi za mapokeo yasiyo na msingi wa Ukweli kama ilivyotabiriwa na kutimiza Maandiko ya Mitume. Kwa hivyo mtu kujulikana kama Mkristo hakumaanishi kuwa unamwamini Mungu.

Thibitisho: "…nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo (2 Timotheo 4:4). "…tena katika ninyi wenyewe watainuka watu, wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao (Matendo 20:30). "Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa" (2 Petro 2:2). "Maana, tazama, giza litaifunika dunia, na giza kuu litazifunika kabila za watu; bali Bwana atakuzukia wewe, na utukufu wake utaonekana juu yako" (Isaya 60:2). "Naye katika mlima huu atauharibu uso wa sitara iliyowekwa juu ya watu wote, na utaji ule uliotandwa juu ya mataifa yote" (Isaya 25:7). "…ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake" (Ufunuo 17:2). "…wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa; wala sauti ya bwana-arusi na bibi-arusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa; maana hao wafanya biashara wako walikuwa wakuu wa nchi, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako" (Ufunuo 18:23).

KUHUSU MAANDIKO

6. Twaweza lupata wapi mafunzo juu ya mapenzi ya Mungu na Ukweli kuhusu Yesu Kristo?

Jibu: Katika Maandiko Matakatifu yanayojulikana nasi kama Biblia.

Thibitisho: "…na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu" (2 Timotheo 3:15). "Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini" (Warumi 15:4). "Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, na kumfahamisha mjinga" (Zaburi 119:130). "…ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii Imani" (Warumi 16:26). "Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu" (Zaburi 119:105).

7. Biblia ni nini?

Jibu: Ni kitabu kilichoandikwa kwa uwezo wa Roho Mtakatiku akifanya kazi katika manabii na mitume walioishi Israel miaka mingi iliyopita. Waliishi nyakati mbalimbali na kuandika kibinafsi lakini wote wakiongozwa na Roho ye yule akiwafunulia nia yake Mungu katika mambo yaliyohusu Historia, maagizo na unabii. Hivyo basi ingawa Biblia imeandikwa na watu mbalimbali, ni Neno la pekee la Mungu.

Thibitisho: "Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki…" (2 Timotheo 3:16). "Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi…" (Waebrania 1:1). "Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni" (1 Wakorintho 2:13). "Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu" (2 Petro 1:21). "Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli" (Yohana 17:17). "Lakini miaka mingi ukachukuliana nao, nawe ukawashuhudia kwa roho yako kwa vinywa vya manabii wako; wao wasitake kusikiliza; kwa hiyo ukawatia katika mikono ya watu wa nchi" (Nehemia 9:30). "Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana" (1 Wakorintho 14:37).

8. Taja majina ya wale walioajiriwa au kutumiwa na Mungu kwa kazi ya uandishi wa Maandiko Matakatifu.

Jibu: Musa, Yoshua, Samweli, Daudi, Sulemani, Isaya, Yeremia, Ezekiel, Danieli, Hosea, Yoabu, Amosi, Obadia, Yona, Mika, Nahumu, Habakuki, Sefania, Hagai, Zekaria, Malaki, Mathayo, Marko, Luka, Yohana, Petro, Yuda, Yakobo, Paulo.

9. Biblia imegawanywa katika sehemu ngapi?

Jibu: Sehemu mbili: Agano la kale na Agano jipya. Lakini katika siku za Yesu, Maandiko yalijulikana kama Musa, Unabii na Zaburi. Agano la Kale liliandikwa na Musa na manabii walikuja baada yake. Agano Jipya liliandikwa na Mitume.

10. Ilichukua muda gani kuandika Biblia kama ilivyo sasa?

Jibu: Agano la Kale lilianza kuandikwa na Musa kama miaka 1600 kabla ya masihi, na kukamilishwa na Malaki miaka 1200 baadaye. (Miaka 400 kabla ya kuzaliwa Kristo). Agano Jipya liliandikwa wakati wa maisha ya Mitume, baada ya kufufuka na kupaa kwake mbinguni, karibu miaka elfu mbili sasa.

11. Biblia ina vitabu vingapi? Taja majina ya vitabu vyenyewa kwa mtiririko.

Jibu: Biblia ina vitabu 66. Vimeorodheshwa hivi: Mwanzo, Kutoka, Mambo ya Walawi, Hesabu, Kumbukumbu la Torati, Yoshua, Waamuzi, Ruthu, 1Samweli, 2 Samweli, 1 Wafalme, 2 Wafalme, 1 Mambo ya Nyakati, 2 Mambo ya Nyakati, Ezra, Nehemia, Esta, Ayubu, Zaburi, Mithali, Mhubiri, Wimbo Ulio Bora, Isaya, Yeremia, Maombolezo, Ezekieli, Danieli, Hosea, Yoeli, Amosi, Obadia, Yona, Mika, Nahumu, Habakuki, Sefania, Hagai, Zekaria, Malaki, Mathayo, Marko, Luka, Yohana, Matendo, Warumi, 1 Wakorintho, 2 Wakorintho, Wagalatia, Waefeso, Wafilipi, Wakolosai, 1 Wathesalonike, 2 Wathesalonike, 1 Timotheo, 2 Timotheo, Tito, Filemoni, Waebrania, Yakobo, 1 Petro, 2 Petro, 1 Yohana, 2 Yohana, 3 Yohana, Yuda, Ufunuo.

12. Biblia katika maandishi yake mbalimbali inatufunulia nini?

Jibu: Biblia, iliyotujia kwa pumzi yake Mungu, inatufunulia kuhusu Mungu na Binadamu.

KUHUSU MUNGU

13. Biblia itafunulia nini kumhusu Mungu?

Jibu: Inatufunulia kuwa kuna Mungu mmoja tu, Baba wa wote, Baba yake Yesu Kristo (Pia), Kwa hivyo, mafunzo ya Utatu hayatokani na Maandiko.

Thibitisho: "Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;…" (1 Timotheo 2:5). "Sikiza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja" (Kumbukumbu la Torati 6:4). ''Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu; nitakufunga mshipi ijapokuwa hukunijua;…" (Isaya 45:5). "…lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake; nasi tunaishi kwake; yuko na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa yeye huyo" (1 Wakorintho 8:6). "Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote;…" (2 Wakorintho 1:3).

14. Biblia inatufunulia nini juu ya hali ya Mungu?

Jibu: Mungu ni mwenye Rehema lakini huitaji amri Yake kufuatwa; Mwenye upendo na huruma lakini ni kama moto unaoangamiza wasiomtii na wenye kiburi; Huwasamehe wakosaji ila huhusudu uwezo wake, utukufu wake, na ukuu wa jina lake. Yeye ni mwenye haki na hawezi kuuangilia uovu. Mungu ni mwenye hekima na hawezi kuwavumilia au kuwafanyia saburi wapumbavu. Yeye ni mwenye ukweli na mwaminifu na atawaondolea mbali waongo na wanafiki. Yeye ni mwenye haki, ukweli na mkamilifu-na pia ni mwenye upendo na mlipizaji kisasi; ana amri au uwezo wa kuua na kufanya hai, mwanzo wa kufanya rehema na kuangamiza kama moto. Yeye anaishi milele, na habadiliki, hafikiwi, hana mwanzo wala mwisho, mtukufu mwenye uwezo na nguvu-mfalme wa milele, mbingu na nchi ni zake, yeye pekee ndiye anayestahili utukufu.

Thibitisho: "…Nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu" (Kutoka 20:6). "Maana Mungu wetu ni moto ulao'' (Waebrania 12:29). "BWANA akapita mbele yake, akatangaza, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;…" (Kutoka 34:6). "Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye;…" (Habakuki 1:13). "…Wajivunao hawatasimama mbele za macho yako; unawachukia wote watendao ubatili. Utawaharibu wasemao uongo; BWANA humzira mwuaji na mwenye hila" (Zaburi 5:5-6). ''Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa" (.Ufunuo 15:3). "Bali BWANA ndiye Mungu wa kweli; ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele; mbele za ghadhabu yake nchi yatetemeka, wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake. Mtawaambia hivi, Miungu hiyo isiyofanya mbingu na nchi, hiyo itaangamia katika nchi, nayo itatoweka chini ya mbingu. Ameiumba dunia kwa uweza wake, ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake, na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu. Atoapo sauti yake, pana mshindo wa maji mbinguni, naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi; huifanyia mvua umeme, huutoa upepo katika hazina zake" (Yeremia 10: 10-13). "Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, yeye ndiye mwenye haki na adili" (Kumbukumbu La Torati 32:4). "Wapenzi, na tupendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo. Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake" (1 Yohana 4:7,8,15). "Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake. Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai" (Waebrania 10:30,31). "Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye, wala hapana Mungu mwingine ila Mimi; naua Mimi, nahuisha Mimi, nimejeruhi, tena naponya; wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu…"(Kumbukumbu La Torati 32:39). "Mimi nitawaponya kurudi nyuma kwao; nitawapenda kwa ukunjufu wa moyo; kwa maana hasira yangu imemwacha. Matawi yake yatatandaa, na uzuri wake utakuwa kama uzuri wa mzeituni, na harufu yake kama Lebanoni" (Hosea 14:4,6). "Wamenitia wivu kwa kisicho Mungu; wamenikasirisha kwa ubatili wao; nami nitawatia wivu kwa wasio watu, nami nitawakasirisha kwa taifa lipumbaalo. Nitaweka madhara juu yao chunguchungu; nitawapiga kwa mishale yangu hata ikaishe;…" (Kumbukumbu La Torati 32:21,23). "Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina" (1 Timotheo 1:17). "Kwa kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo" (Malaki 3:6). "BWANA ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana, wala ukuu wake hautambulikani (Zaburi 145:3). "Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu, akili zake hazina mpaka" (Zaburi 147:5). "Ee BWANA, kutukuza usitutukuze sisi, bali ulitukuze jina lako, kwa ajili ya fadhili zako, kwa ajili ya uaminifu wako" (Zaburi 115:1). "Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi" (Mwanzo 14:19).

15. Je, Mungu anaishi tu Mbinguni?

Jibu: La. Yu kila mahali na hakuna kisichodhihirika machoni pake.

Thibitisho: "Je, mtu ye yote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? asema BWANA. Je! mbingu na nchi hazikujawa nami? asema BWANA" (Yeremia 23:24). "Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu" (Waebrania 4:13). "Ee BWANA, umenichunguza na kunijua. Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu; umelifahamu wazo langu tokea mbali. Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, umeelewa na njia zangu zote. Maana hamna neno ulimini mwangu usilolijua kabisa, BWANA" (Zaburi 139:1-4).

KUHUSU ROHO YA MUNGU

16. Mungu anawezaje kuwa kila mahali ikiwa makao yake ni mbinguni?

Jibu: Mungu yu kila mahali kwa Roho yake ambayo yatoka kwake na kusambaa kotekote.

Thibitisho: "Waipeleka roho yako, wanaumbwa, nawe waufanya upya uso wa nchi" (Zaburi 104:30). "Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko" (Zaburi 139:7,8).

17. Roho ya Mungu ni nini?

Jibu: Ni nguvu Zake zisizoonekana inayopulizwa kutoka Kwake na ni sawa na hali yake ya utukufu. Kwa njia hii mbingu na nchi zimeumbwa na kuimarishwa na kuhifadhiwa toka zama za zama. Kwa njia hii twaishi na kuenenda na twahifadhiwa na kuwa na hali tuliyonayo.

Thibitisho: "Roho ya Mungu imeniumba, na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai" (Ayubu 33:4). "Hizo mbingu hupambwa kwa roho yake; mkono wake umemchoma nyoka aendaye mbio" (Ayubu 27:13). "…waipeleka roho yako, wanaumbwa, nawe waufanya upya uso wa nchi" (Zaburi 104:30). "Kwa neno la BWANA mbingu zilifanyika, na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake" (Zaburi 33:6). "Aa! Bwana MUNGU, tazama, wewe umeziumba mbingu na nchi, kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyoshwa; hapana neno lililo gumu usiloliweza;…" (Yeremia 32:17). "Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji" (Mwanzo 1:2). "Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake" (Matendo 17:28). "Kama akimwekea mtu moyo wake, Akijikusanyia roho yake na pumzi zake; wenye mwili wote wataangamia pamoja, nao wanadamu watarejea tena kuwa mavumbi" (Ayubu 34:14,15).

18. Je, Mungu ni mbali na Roho ya Mungu?

Jibu: La hasha! Mungu na Roho yake sio mbali. Wao ni kitu kimoja. Kama vile jua na miali ya jua ilivyo moja. Kwa hivyo Roho inayotokana na Mungu ni kitu kimoja Naye. Mungu ni kiini na kilele cha utukufu wa Roho inayojaza dunia.

Thibitisho: "Nikaribieni, sikieni haya; tokea mwanzo sikunena kwa siri; tangu yalipokuwapo mimi nipo; na sasa Bwana MUNGU amenituma, na roho yake" (Isaya 48:16). "BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini" (Mwanzo 6:3). "Je, mtu ye yote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? asema BWANA. Je! mbingu na nchi hazikujawa nami? asema BWANA"(Yeremia 23:24). "Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako?" (Zaburi 139:7). "Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli" (Yohana 4:24).

19. Je, mambo haya yanakufunza cho chote kuhusu mwenendo wako?

Jibu: Ndio! Yananifunza kuwa kila mara ni machoni pa Mungu. Ingawa sihisi, na kuwa ananiona kila wakati (hata wakati wa giza totoro) ingawa mimi simwoni. Hakuna kinachoweza kutendeka bila yeye kufahamu. Hata mawazo yangu ya ndani anayatambua hata nikijaribu kuyaficha.

Thibitisho: "Akaliita jina la BWANA aliyesema naye, Wewe U Mungu uonaye, kwani alisema, Hata hapa nimemwona yeye anionaye?" (Mwanzo 16:13). "Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu" (Waebrania 4:13). "…giza nalo halikufichi kitu, bali usiku huangaza kama mchana; giza na mwanga kwako ni sawasawa" (Zaburi 139:12). "Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo (Waebrania 4:12).

KUHUSU MWILI WA KIROHO

20. Mwili wa kiroho ni wa aina gani?

Jibu: Ni mwili uliofanyika kwa mfano wa hali ya Mungu ukiwa na Roho ya Mungu, na kwa hivyo hauharibiki na ni wa milele.

Thibitisho: "…hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko. Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho" (1 Wakorintho 15:44-46). "Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho" (Yohana 3:6). "Lakini, ikiwa Roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu" (Warumi 8:11). "Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni" (1 Wakorintho 15:49). "Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa" (1 Wakorintho 15:53). "…atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uwezo ule ambao kwa huo uwezo hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake" (Wafilipi 3:21).

21. Je, mwili wa kiroho ni sawa na mwili wa milele?

Jibu: Ni kama huo kwa hali lakini sio kimaumbile.

Thibitisho: "Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa" (1 Wakorintho 15:51-53). "…wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni" (Matendo 1:11). "Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo" (Luka 24:39). "Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo" (1 Yohana 3:2).

22. Ni nini tofauti iliyoko kati ya maumbile ya mwili wa kiroho na wa kufa?

Jibu: Mwili wa kufa huja ukachakaa na kufa; lakini mwili wa kiroho ni wa milele. Mwili wa kufa ni dhaifu, mwili wa kiroho ni wenye nguvu; mwili wa kufa ni wenye kuchakaa, usionawiri na usi ona utukufu au hadhi, hali mwili wa kiroho hauchakai, unanawiri na umetukuka. Na hata mavazi yaliyov yalishwa mwili wa kiroho yaweza kuwa meupe kama theluji na kung'ara kama jua.

Thibitisho: "…wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo" (Luka 20;36). "Kadhalika na kiyama ya wafu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika;…" (1Wakorintho 15 :42). "Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote." (Ufunuo 7:16). "Je! mimi si huru? mimi si mtume? mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? ninyi si kazi yangu katika Bwana?" (1 Wakorintho 9:1). "Ee Mfalme, ndipo wakati wa adhuhuri njiani naliona nuru inatoka mbinguni ipitayo mwangaza wa jua, ikinimulikia mimi, na wale waliofuatana nami pande zote" (Matendo 26:13). "…akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang'aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru" (Mathayo 17:2). "Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji" (Mathayo 28:3). "…bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia" (Isaya 40:31). "Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele" (Danieli 12:3).

23. Tutaweza kubadilishiwa miili yetu hii ya kufa iwe ya kiroho?

Jibu: Wote wanoamini Ukweli watashiriki mwili wa kiroho, wale wanaotii amri na kuvumilia hadi mwisho. Watafufuliwa toka kuzimu kwa kuja kwake Kristo na waje mbele yake kwa hukumu pamoja na wengine wote wakati huo ambao wameletwa mbele ya kiti cha hukumu. Akisha watenga kutoka kwa wasiowaaminifu, wasiowaaminifu wataondolewa mbele yake ili wataharike, waangamie, wafe, na hali wale waliokubaliwa watageuzwa, wote pamoja kufumba na kufumbua, kuwa sawa na hakimu wao mtukufu.

Thibitisho: "Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,…" (1 Wakorintho 15:51). "Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya" (2 Wakorintho 5:10). "Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele" (Wagalatia 6:8). "Lakini, ikiwa Roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu Basi, kama ni hivyo, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili; kwa maana kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Kwa kuwa hamkupokea tena roho ya utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye" (Warumi 8:11-17). "Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele" (Danieli 12:2). "Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?" (Mathayo 7:22). "Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu, bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele" (Wagalatia 6:8). "Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele" (Mathayo 25:46). "…watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake;…" (2 Wathesalonike 1:9).

KUHUSU MALAIKA

24. Malaika ni akina nani?

Jibu: Ni viumbe vyenye utukufu vinavyotumwa miisho ya ulimwengu.

Thibitisho: "Mhimidini BWANA, enyi malaika zake, ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, mkiisikiliza sauti ya neno lake" (Zaburi 103:20). "Umemfanya mdogo punde kuliko malaika, umemvika taji ya utukufu na heshima, umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;…" (Waebrania 2:7). "Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi" (Mwanzo 19:1). "…naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni. Akaniagiza, akaongea nami, akasema, Ee Danieli, nimetokea sasa, ili nikupe akili upate kufahamu. Mwanzo wa maombi yako ilitolewa amri, nami nimekuja kukupasha habari; maana wewe unapendwa sana; basi itafakari habari hii, na kuyafahamu maono haya" (Danieli 9:21-23). "Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,…" (Luka 1:26). "Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu. Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana. Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng'ombe. Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema, Atukuzwe Mungu juu mbinguni, na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia" (Luka 2:9-14). "Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;…" (Mathayo 25:31). "Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,…" (Ufunuo 5:11).

25. Maumbile ya malaika yakoje?

Jibu: Wana miili ya kiroho lakini wafanana na binadamu.

Thibitisho: "Huwafanya malaika zake kuwa pepo, na watumishi wake kuwa moto wa miali" (Zaburi 104:4). "Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua" (Waebrania 13:2). "Malaika wa BWANA akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; likini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume. Basi Manoa akainuka, akamwandama mkewe, na kumfikilia mtu huyo, akamwuliza, Je! wewe ndiwe mtu yule aliyenena na huyu mwanamke? Akasema, Naam, ni mimi. Lakini malaika wa BWANA akamwambia Manoa, Ujapokuwa wanizuia, sitakula katika mkate wako; na kwamba wataka kufanya tayari sadaka ya kuteketezwa, inakupasa kumsongezea BWANA. Kwa kuwa Manoa hakujua ya kwamba yeye ni malaika wa BWANA. Kwa maana, ikawa, mara huo mwali wa moto ulipopaa juu mbinguni kutoka pale madhabahuni, huyo malaika wa BWANA akapaa katika mwali wa moto wa madhabahu, nao Manoa na mkewe wakaangalia; wakapomoka nchi kifudifudi. Lakini malaika wa BWANA hakumtokea Manoa tena, wala mkewe. Ndipo Manoa alipojua ya kwamba ndiye malaika wa BWANA" (Waamuzi 13:3, 11, 16, 20, 21). "Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia" (Mathayo 28:2). "Wakaingia kaburini wakaona kijana ameketi upande wa kuume, amevaa vazi jeupe; wakastaajabu" (Marko 16:5).

26. Je, malaika wana maumbile sawa na vile tutakavyokuwa siku zijazo? Ikiwa tutaokolewa wakati wa ufufuo?

Jibu: Ndio. Tutakuwa hivo hivyo kwa kila hali. Ahadi ni kuwa tutakuwa sawa nao, na tusife tena.

Thibitisho: "…lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi;…" (Luka 20:35).

27. Malaika wamewahi kuonekana duniani?

Jibu: Ndio. Tena mara nyingi. Watatu walijidhihirisha kwa Ibrahimu; wawili wakaenda Sodoma; mmoja alishindana na Yakobo, ambaye pia aliona kaumu yao; mmoja aliwaongoza wana wa Israel kutoka Misri; mmoja akamzuia Baalam; mmoja alijidhihirisha kwa Gidion, mwingine kwa Manoa, mwingine kwa Daudi, Danieli, mmoja akaangamiza Jeshi la Sennakerebu; mwingine alijitokeza kwa baba yake Yohana; mmoja kwa mama yake Yesu; mwingine kwa wachungaji; umati wao walionekana wakiimba. Na pia walijitokeza wakati wa ufufuo wa Kristo. Na mahali mbali mbali kwa mitume baada ya kupaa kwa Kristo.

Thibitisho: "BWANA akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari" (Mwanzo 18:1). "Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi" (Mwanzo 19:1). "Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri" (Mwanzo32:24). "Naam, alikuwa na uwezo juu ya malaika akashinda; alilia, na kumsihi; alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko;…" (Hosea 12:4). "Yakobo akashika njia yake na malaika wa Mungu wakakutana naye" (Mwanzo 32:1). "Kisha malaika wa Mungu, aliyetangulia mbele ya jeshi la Israeli, akaondoka akaenda nyuma yao; na ile nguzo ya wingu ikaondoka hapo mbele yao, ikasimama nyuma yao; ikafika kati ya jeshi la Misri na jeshi la Israeli; napo palikuwa na lile wingu na lile giza, lakini lilitoa nuru wakati wa usiku; na hawa hawakuwakaribia hawa usiku kucha. Musa akanyosha mkono wake juu ya bahari; BWANA akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu, maji yakagawanyika. Wana wa Israeli wakaenda ndani kati ya bahari katika nchi kavu; nayo maji yalikuwa ukuta kwao mkono wa kuume, na mkono wa kushoto. Na wale Wamisri wakawafuatia, wakaingia ndani kati ya bahari, farasi zote za Farao, na magari yake, na wapanda farasi wake. Ikawa katika zamu ya alfajiri, BWANA akalichungulia jeshi la Wamisri katika ile nguzo ya moto na ya wingu, akalifadhaisha jeshi la Wamisri" (Kutoka 14:19-24). "Hasira ya Mungu ikawaka kwa sababu alikwenda; malaika wa BWANA akajiweka njiani, ili kumpinga. Basi alikuwa amepanda punda wake, na watumishi wake wawili walikuwa pamoja naye" (Hesabu 22:22). "Malaika wa BWANA akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani"(Waamuzi 6:11). "Malaika wa BWANA akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume. Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi; kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti. Ndipo yule mwanamke akaenda akamwambia mume wake, akisema, Mtu wa Mungu alinijia, na uso wake ulikuwa kama uso wa malaika wa Mungu, wa kutisha sana; nami sikumwuliza, Umetoka wapi? wala hakuniambia jina lake; lakini aliniambia, Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; basi sasa, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hata siku ya kufa kwake. Ndipo huyo Manoa akamwomba BWANA, akisema, Ee Bwana, nakuomba, yule mtu wa Mungu uliyemtuma na aje kwetu mara ya pili, atufundishe hayo yatupasayo kumfanyia huyo mtoto atakayezaliwa. Mungu akasikiza sauti ya Manoa; naye malaika wa Mungu akamwendea yule mwanamke tena alipokuwa anaketi shambani; lakini mumewe, Manoa, hakuwapo pamoja naye. Basi huyo mwanamke akaenda haraka, akapiga mbio, na kumwambia mumewe, akisema, Tazama, huyo mtu amenitokea, huyo aliyenijilia siku ile. Basi Manoa akainuka, akamwandama mkewe, na kumfikilia mtu huyo, akamwuliza, Je! wewe ndiwe mtu yule aliyenena na huyu mwanamke? Akasema, Naam, ni mimi. Manoa akasema, Basi sasa hayo maneno yako yatakapotimia, je! huyo mtoto atakuwa wa namna gani, na kazi yake itakuwa ni nini? Malaika wa Mungu akamwambia Manoa, Katika hayo yote niliyomwambia huyo mwanamke na ajihadhari. Asile kitu cho chote kitokacho katika mzabibu, wala asinywe divai, wala mvinyo, wala asile kitu cho chote kilicho najisi; hayo yote niliyomwamuru na ayatunze. Kisha Manoa akamwambia huyo malaika wa BWANA, Nakuomba, tukuzuie, ili tupate kuandaa mwana-mbuzi kwa ajili yako. Lakini malaika wa BWANA akamwambia Manoa, Ujapokuwa wanizuia, sitakula katika mkate wako; na kwamba wataka kufanya tayari sadaka ya kuteketezwa, inakupasa kumsongezea BWANA. Kwa kuwa Manoa hakujua ya kwamba yeye ni malaika wa BWANA" (Waamuzi 13:3-16). "Lakini huyo malaika aliponyosha mkono wake kuelekea Yerusalemu ili auharibu, BWANA akaghairi katika mabaya, akamwambia huyo malaika mwenye kuwaharibu watu, Yatosha, sasa ulegeze mkono wako. Naye yule malaika wa BWANA alikuwako karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi" (2 Samweli 24:16). "…naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni" (Danieli 9:21). "Nami, Danieli, nikaona maono haya peke yangu; maana wale watu waliokuwa pamoja nami hawakuyaona maono haya; lakini tetemeko kuu liliwashika, hata wakakimbia ili kujificha. Basi nikaachwa peke yangu, nikaona maono haya makubwa, wala hazikubaki nguvu ndani yangu; maana uzuri wangu uligeuzwa ndani yangu kuwa uharibifu, wala sikusaziwa nguvu. Walakini naliisikia sauti ya maneno yake; nami niliposikia sauti ya maneno yake, ndipo nikashikwa na usingizi mzito, na uso wangu umeielekea nchi. Na tazama, mkono ukanigusa, ukaniweka juu ya magoti yangu, na vitanga vya mikono yangu. Akaniambia, Ee Danieli, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame kiwima-wima; maana kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neno hili, nalisimama nikitetemeka. Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kuinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako" Danieli 10:7-12). "Ikawa usiku uo huo malaika wa BWANA alitoka, akakiingia kituo cha Waashuri, akawapiga watu mia na themanini na tano elfu. Na watu walipoondoka asubuhi na mapema, kumbe! hao walikuwa maiti wote pia" (2 Wafalme 19:35). "Akatokewa na malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia. Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia. Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana. Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake. Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye. Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao. Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa. Zakaria akamwambia malaika, Nitajuaje neno hilo? maana mimi ni mzee, na mke wangu ni mkongwe wa siku nyingi. Malaika akamjibu akamwambia, Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu; nami nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema. Na tazama! utakuwa bubu, usiweze kusema, mpaka siku ile yatakapotukia hayo, kwa sababu hukuyasadiki maneno yangu; nayo yatatimizwa kwa wakati wake. Na wale watu walikuwa wakimngojea Zakaria, wakastaajabia kukawia kwake mle hekaluni. Alipotoka hali hawezi kusema nao, walitambua ya kuwa ameona maono ndani ya hekalu, naye aliendelea kuwaashiria akakaa bubu. Ikawa siku za huduma yake zilipokuwa zimetimia akaenda nyumbani kwake. Hata baada ya siku zile mkewe Elisabeti alichukua mimba akatawa miezi mitano, akisema, Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana katika siku zile alizoniangalia ili kuniondolea aibu yangu mbele ya watu. Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,…" (Luka 1:11-26). "Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia" (Mathayo 28:2). "Ikawa walipokuwa wakifadhaika kwa ajili ya neno hilo, tazama, watu wawili walisimama karibu nao, wamevaa nguo za kumetameta;…" (Luka 24:4). "Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe,…" (Matendo 1:10). "…lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema,…" (Matendo 5:19). "Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi. Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate. Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni kweli yaliyofanywa na malaika; bali alidhani kwamba anaona maono. Na walipopita lindo la kwamza na la pili, wakaja hata mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia wenyewe. Wakatoka nje, wakapita katika njia moja; mara malaika akamwacha. Hata Petro alipopata fahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na katika kutazamia kote kwa taifa la Wayahudi" (Matendo 12:7-11). "Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana;…" (Ufunuo 1:1). "Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi; ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi" (Ufunuo 22:16).

28. Je, Malaika wana majina?

Jebu: Ndio. Kama vile Gabriel; lakini jina linalotumiwa kwao katika Biblia ni Malaika tu. Wakati mwingine wanatajwa kama kwamba ni Mungu.

Thibitisho: "Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,…" Luka 1:26). "Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee" (Yuda 9). "Yakobo akamwuliza, akasema, Niambie, tafadhali, jina lako? Akasema, Kwa nini waniuliza jina langu? Akambariki huko. Yakobo akapaita mahali pale, Penueli, maana alisema, Nimeonana na Mungu uso kwa uso, na nafsi yangu imeokoka" Mwanzo 32:29-30). "Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa" (Mwanzo 31:13). "Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea. Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei. BWANA alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa. Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu. Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu" (Kutoka 3:2-6).

29. Kwa nini malaika wanatajwa kana kwamba ni Mungu?

Jibu: Kwa sababu wanashughulikia kazi ya Mungu na kuenenda kwa nguvu Zake na pia kwa sababu wana maumbile yaliyo sawa. Jina lake (Mungu) li ndani yao.

Thibitisho: Tazama majibu ya 24-26. "Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea. Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kisirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake" (Kutoka 23: 20-21).

KUHUSU BINADAMU

30. Biblia yatufunulia nini kumhusu binadamu?

Jibu: Biblia yatufunulia kuwa binadamu ni kiumbe chenye nafsi hai, aliyetokana na mavumbi ya ardhi, na kuumbwa na Mungu.

Thibitisho: "BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai" (Mwanzo 2:7). "Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba" (Mwanzo 1:27). "…kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi" (Mwanzo 3:19). "Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi" (Zaburi 103:14). "Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu" (Mwanzo 18:27).

31. Je, binadamu ni kiumbe chenye uhai wa milele?

Jibu: La hasha! Ni kiumbe cha kufa. Hufa na kurudia mavumbi.

Thibitisho: "Lakini mwanadamu hufa, huifariki dunia; naam, mwanadamu hutoa roho, naye yupo wapi?" (Ayubu 14:10). "…Je! binadamu atakuwa na haki kuliko Mungu? Je! mtu atakuwa safi kuliko Muumba wake? (Ayubu 4:17). "Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili. Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena" (Mhubiri 3 19-20). "Ni mwanamume gani atakayeishi asione mauti, atakayejiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu? (Zaburi 89:48).

32. Je, kuna sehemu au chembe fulani ya binadamu iliyo na uhai wa milele, kama wanavyoamini madhehebu mbalimbali ulimwenguni kote?

Jibu: La: mafundisho hayo ni mojawapo ya hadaa au uongo ambao umechukuliwa kama ukweli. Binadamu ni kiumbe kinachokufa kabisa! Ni Mungu pekee ndiye aliye na uzima wa milele. Uzima wa milele ni kitu ambacho binadamu anapaswa kutafuta. Ni jambo la ahadi na Tumaini.

Thibitisho: "Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,…" (Mwanzo 3:4). "Ee BWANA, nguvu zangu, ngome yangu, na kimbilio langu siku ya taabu, kwako wewe watakuja mataifa yote toka ncha za dunia, wakisema, Baba zetu hawakurithi kitu ila uongo, naam, ubatili na vitu visivyofaa" (Yeremia 16:19). "…ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina" (1 Timotheo 6:16). "Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina" (1 Timotheo 1:17). "…wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, watapewa uzima wa milele;…" (Warumi 2:7)."…na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili;…" (2 Timotheo 1:10). "…katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele;…" (Tito 1:2). "Na hii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani, uzima wa milele" (1 Yohana 2:25).

33. Je, uhai wa mtu hauwezi kuwa hai hata kama mwili wake hufa?

Jibu: Uhai wa mtu haumo ndani ya mtu kibinafsi. Ni nguvu za Mungu zinazomfanya kuwa hai. Na humrudia Mungu binadamu anapofariki. Kama Mungu angekusanya uhai huu binadamu angetokomea asiwepo tena.

Thibitisho: "Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima, katika nuru yako tutaona nuru" (Zaburi 36:9). "…wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote" (Matendo 17:25). "Ambaye nafsi ya kila kilicho hai i mkononi mwake, na pumzi zao wanadamu wote" (Ayubu 12:10). "…Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa" (Mhubiri 12:7). "Kama akimwekea mtu moyo wake, akijikusanyia roho yake na pumzi zake;…" (Ayubu 34:14). "Mwacheni mwanadamu ambaye pumzi yake i katika mianzi ya pua yake; kwa maana hudhaniwaje kuwa ni kitu?" (Isaya 2: 22).

34. Basi, kwani binadamu hana kumbukumbu au chembe cha uhai katika mauti?

Jibu: Binadamu hana chembe cha uhai katika mauti. Amekufa amekufa kabisa. Kwa muda huo, hafahamu cho chote kama vile mtoto ambaye hajazaliwa.

Thibitisho: "…kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa: (Mhubiri 9:5). "Maana mautini hapana kumbukumbu lako; katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?" (Zaburi 6:5). "Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe" (Mhubiri 9:10). "Msiwatumainie wakuu, wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake. Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, siku hiyo mawazo yake yapotea" (Zaburi 146:3-4). "Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako. Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo; baba atawajulisha watoto kweli yako" (Isaya 38:18-19). "Kwa nini basi kunitoa tumboni? Ningekata roho, lisinione jicho lo lote. Ningalikuwa kama mtu asiyekuwapo; ningalichukuliwa kaburini kutoka tumboni" (Ayubu 10:18-19).

35. Kwa nini binadamu yumo katika hali hii ya uovu na ya kufa?

Jibu: Mtu ni kiumbe cha kufa kwa sababu ya dhambi. Ni sheria ya Mungu kuwa wenye dhambi hawana budi kufa. Adam, baba wetu, alitenda dhambi na akahukumiwa kifo kabla hajawa na watoto. Mauti yalitokana naye, na yakatujia kwa sababu yake yeye, twapokea maumbile yale yaliyo asili yake, baada ya kuhukumiwa kufa. Hivi basi twashiriki hukumu ya kifo chake. Mbali na haya, sisi wenyewe ni wenye dhambi.

Thibitisho: "Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu" (Warumi 6:23). "Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;…" (Warumi 5:12). "Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi" (Mwanzo 3:17-19). "Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa" (1 Wakorintho 15:22). "Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima" (Warumi 5:18). "…kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;…" (Warumi 3:23). "Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu; ili tusijitumainie nafsi zetu, bali tumtumaini Mungu, awafufuaye wafu,…" (2 Wakorintho 1:9). "Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa" (1 Wakorintho 15:53). "Ole wangu, maskini mimi! ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?" (Warumi 7:24). "Kwa maana sisi tulio hai, sikuzote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu ipatikanayo na mauti" (2 Wakorintho 4:11).

36. Je, Mungu anakusudia kuwa wanadamu wataendelea kuwa katika hali hii ya uovu?

Jibu: La: Anakusudia kuondoa dhambi kutoka duniani kabisa, na aangamize mauti isiwepo.

Thibitisho: "Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? kujuta kutafichwa na macho yangu" (Hosea 13:14). "Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana BWANA amenena hayo" (Isaya 25:8). "Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita" (Ufunuo 21:4). "Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti" (1 Wakorintho 15:26). "Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!" (Yohana 1:29). "…na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili;…"(2 Timotheo 1:10).

37. Mungu atafanyiza mabadiliko haya makuu bila kujali kama wanadamu wanamtii?

Jibu: La: Kazi itafanywa kwa haki. Kama vile mauti yalivyokuja kwa njia ya dhambi, kutotii, hivyo basi uzima utakuja kwa kazi ya kutenda haki, yaani kwa utii.

Thibitisho: "Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki" (Warumi 5:19). "Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na manabii; ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti;…" (Warumi 3:21-22). "Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,…" (1 Wakorintho 6:9). "Na mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi?" (1 Petro 4:18). "Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna" (Wagalatia 6:7). "Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni" (Mathayo 5:20).

38. Biblia inaeleza kinagaubaga kuwa hakuna aliye haki. Basi wokovu utakujaje kutokana na kazi ya kutenda haki?

Jibu: Hali ya binadamu akiachwa kujikatia kauli ndivyo Biblia isemavyo. Lakini Mungu hajamtupilia mbali binadamu. Amejishughulisha na mambo yake na amefungulia njia ya kutenda haki na anawaita wanadamu kuifuata njia hiyo. Mungu ameuleta wokovu karibu kupitia kwa Yesu Kristo na anawauliza watu waufuate kwa kuwa na imani katika yeye.

Thibitisho: "Akaona ya kuwa hapana mtu, akastaajabu kwa kuwa hapana mwombezi; basi, mkono wake mwenyewe ndio uliomletea wokovu; na haki yake ndiyo iliyomsaidia" (Isaya 59:16). "Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima" (Warumi 5:18). "Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;…" (1 Wakorintho 1:30). "Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu. Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki" (Warumi 9:3-4).

39. Inawezekanaje, binadamu ambaye amekuwa ni mwenye dhambi aupate wokovu ulio katika Kristo?

Jibu: Kwa sababu Mungu anawataka wanadamu wote watubu na yu tayari kusamehe dhambi ikiwa ataamini na kumvaa Kristo kwa imani.

Thibitisho: "Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu" (Matendo 17:30). "Basi, na ijulikane kwenu, ndugu zangu, ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi;…" (Matendo 13:38). "…mtu mbaya na aache njia yake, na mtu asiye haki aache mawazo yake; na amrudie BWANA, naye atamrehemu; na arejee kwa Mungu wetu, naye atamsamehe kabisa" (Isaya 55:7). "Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu: (Matendo 2:38). "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo" (Matendo 4:12).

40. Je, hawa wanaokolewa kwa imani tu katika Kristo?

Jibu: La: Imani yakusahaulisha na dhambi za awali, na inakupa uhakikisho wa mapatano ya amani na Mungu wako; lakini kazi au matendo ni lazima ili kupata ukamilisho wa imani na kukubalika hatimaye.

Thibitisho: "Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo" (Warumi 5:1). "Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke" (1 Wakorintho 10:12). "…kwa maana kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi" (Warumi 8:13). "Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza" (2 Petro 2:20). "Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake" (Yakobo 2:24). "Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu" (Ufunuo 2:5). "…nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake" (Ufunuo2:23).

KUHUSU KRISTO

41. Yesu Kristo alikuwa nani?

Jibu: Yesu Kristo alikuwa mwana wa Mungu.

Thibitisho: "…na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye" (Mathayo 3:17). "…je! yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?" (Yohana 10:36). "Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli" (Yohana 1:49). "Basi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu" (Marko 15:39). "Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu" Yohana 1:34).

42. Je, Yesu Kristo alikuwa binadamu na kwa wakati huo huo mwana wa Mungu?

Jibu: Ndio. Alikuwa binadamu pia. Aliyefanyika katika kila njia kama sisi, bali hakutenda dhambi.

Thibitisho: "Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;…" (Matendo 2:22). "Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;…" (1 Timotheo 2:5). "Basi, na ijulikane kwenu, ndugu zangu, ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi;…" (Matendo 13:38). "Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake" (Waebrania 2:17).

43. Yesu Kristo alikuwaje mwana wa Mungu na pia binadamu?

Jibu: Kwa sababu alizaliwa kwa nguvu za Mungu kupitia kwa mwanamke bikira pasipo na mume. Mariam, msichana aliyetokana na uza o wa Daudi, aliyekuwa mchumba wa Yusufu ambaye pia ni wa mbari ya Daudi, alikuwa mama wake, na Mungu baba yake. Kwa hivyo kwa upande wa baba, Mungu alikuwa baba yake, na kwa upande wa mama alikuwa mwana wa Daudi, na kwa hivyo, Yesu ametokana na Daudi na kuchvkua au kurithi maumbili ya Daudi, maumbili ambayo ni ya kibinadamu.

Thibitisho: "Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu" (Mathayo 1:20). "Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu" (Luka 1:35). "Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu" (Mathayo 1:1). "Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtima Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria,…" (Wagalatia 4:4). "…tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadame, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba" (Wafilipi 2:8). "Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi" (Waebrania 4:15).

44. Je, Yesu alikuwa na uungu na vile vile ubinadamu?

Jibu: Alikuwa binadamu kutokana na hali ya mwili bali alikuwa na uungu uliotokana na asili ya kuwako kwake. Roho iliyompa hekima aliyokuwa nayo, na hali ya mwenendo aliokuwa nao. Ilitokana na asili ya huo uungu.

Thibitisho: "Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilishi,…" (Waebrania 2:14). "Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka" (Yohana 6:38). "Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake" (Luka 2:40). "Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli" (Yohana 1:14).

45. Je, kulikuwepo na uhusiano fulani kati ya Yesu na Baba yake ambayo haipo kati yake Mungu na wanadamu wengine?

Jibu: Ndiyo. Yesu na Baba walikuwa wamoja kwa roho, ambayo, ilitoka kwa Mungu, iliwaambatanisha wote wawili, kwa Mungu alikuwa katika Kristo, na hivyo basi Kristo alikuwa ndio udhihirisho wa Mungu: mambo ambayo hayamgusi mtu awaye yote.

Thibitisho: "Mimi na Baba tu umoja" (Yohana 10:30). "Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba? Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake" (Yohana 14:9-10). "…yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho" (2 Wakorintho 5:19). "Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, akajulika kuwa na haki katika roho, akaonekana na malaika, akahubiriwa katika mataifa, akaaminiwa katika ulimwengu, akachukuliwa juu katika utukufu" (1 Timotheo 3:16).

46. Je, Yesu alikuwa Mungu, nguvu sawa na aliyeishi tangu hapo na Mungu, kama wanavyosema wanaoamini na kufunza Utatu?

Jibu: Mwanadamu Yesu Kristo, mwana wa pekee wa Mungu, aliyepewa uwezo wa Roho bila kipimo, alikvwani mbali na baba, ingawa wamoja kama ilivyoelezwa katika jibu la awali. Juu ya kuwa na nguvu sawa na kuishi pamoja tangu hapo. Haya ni maoni au rai na majadiliano ya walimuwa dini wa makanisa katika karne ya tatu na nne. Mafunzo haya ya utatu hayana asili yake katika mafunzo ya mitume karne ya kwanza au wakati Yesu alipokuwepo. Mkondo huu wa mafunzo wahubiri kuwa Mungu wa Kristo alikuwa baba anayejaza mbingu na nchi. Kristo alikana kuwa yeye alikuwa na nguvu sawa na baba; na nguvu sawa haiwezekani kwa mwana kuwa nayo.

Thibitisho: Thibitisho 41-45. "Mimi ndimi ninayejishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenipeleka ananishuhudia" (Yohana 8:18). "Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe" (Yohana 14:11). "Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba; kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi" (Yohana 14:28). "Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu" (1 Wakorintho 11:3). "Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote" (1 Wakorintho 15:28).

KUHUSU JINA LA YESU

47. Kwa nini Yesu aliitwa jina hilo?

Jibu: Kuonyesha alikuwa nani na kazi aliyotumwa kuifanya.

Thibitisho: "Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao" (Mathayo 1:21).

48. Ni kwa njia gani jina hili la tuonyesha haya?

Jibu: Kwanza, maana ya Yesu, asili yake ikiwa ni Kiyunani, ni Mungu Ataokoa; na kwa Kristo, ambalo ni neno la kiyunani, ina maana ya mpakwa mafuta.

Thibitisho: "Tazama, bikira atachukua mimba, naye atazaa mwana; nao watamwita jina lake Imanueli: Yaani, Mungu pamoja nasi" (Mathayo 1:23). "Wafalme wa dunia wanajipanga, na wakuu wanafanya shauri pamoja, juu ya BWANA, na juu ya masihi wake,…" (Zaburi 2:2). "Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,…" (Matendo 4:27).

49. Kupakwa mafuta maana yake nini?

Jibu: Ni njia ambayo wafalme na makuhani waliweza kupewa mamlaka. Walitawazwa kwa kupakwa mafuta matakatifu.

Thibitisho: "Ndipo utakapotwaa hayo mafuta ya kutiwa, na kummiminia kichwani mwake, na kutia mafuta. Kisha walete hao wanawe na kuwavika kanzu" (Kutoka 29:7-9). "…Kesho, wakati kama huu, nitakuletea mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe mtie mafuta ili awe mkuu juu ya watu wangu Israeli; naye atawaokoa watu wangu na mikono ya Wafilisti; maana nimewaangalia watu wangu, kwa sababu kilio chao kimenifikilia" (1 Samweli 9:16). "Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu akasema, Je! BWANA hakukutia mafuta uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa BWANA, na kuwaokoa na mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa BWANA amekutia mafuta uwe mkuu juu ya urithi wake: (1 Samweli 10:1). "BWANA akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe. Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari, ataniua. Basi BWANA akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili kumtolea BWANA dhabihu. Ukamwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuoyesha utakayotenda; nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako" (1 Samweli 16:1-3).

50. Je, Kristo alipakwa mafuta?

Jibu: La hasha. Alitawazwa na kile ambacho mtindo wa awali ulikuwa mfano wake. Alitawazwa kwa Roho wa Mungu wakati wa vbatizo wake Yordani.

Thibitisho: "…habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu; naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye" (Matendo 10:38). "Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka; Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe" (Luka 3:21-22).

51. Kwa hivyo mtu ambaye angekuwa na jina hilo la Yesu Kristo angetumiwa na Mungu, kama chombo cha kuokoa binadamu-kutoka kwa nini?

Jibu: Kutoka kwa dhambi zao.

Thibitisho: "Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao" (Mathayo 1:21).

KUHUSU KIFO CHA KRISTO

52. Ni kwa njia gani Mungu anawaokoa binadamu kutoka kwa dhambi zao katika Kristo?

Jibu: Anawasamehe kwa ajili ya Kristo, na kwa nguvu ya mahubiri. Anawageuza watu kutoka kwa njia zao za dhambi na kuwaongoza kwenye njia ya haki.

Thibitisho: "…tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi" (Waefeso 4:32). ":ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;…" (Wakolosai 1:14). "Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake" (1 Yohana 2:12). "Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake" (Matendo 3:26).

53. Kwa nini Mungu anasamehe kwa ajili ya Kristo?

Jibu: Kwa sababu ya yale yaliyoweza kutimizwa katika yeye.

Thibitisho: "Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, na kuwaombea wakosaji" (Isaya 53:12).

54. Ni mambo gani yaliyotimizwa katika Kristo?

Jibu: Dhambi imehukumiwa katika mauti yake. Juu ya mti na haki yake Mungu imedhihirishwa na kuonyeshwa kwa ulimwengu mzima katika umwagikaji wa damu yake.

Thibitisho: "Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu" (Warumi 6:10). "Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti; ili, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa" (1 Petro 2:24). "Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;…" (Warumi 8:3). "ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake, ili aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa; apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yeye amwaminiye Yesu" (Warumi 3:25-26).

55. Dhambi ingewezaje kuhukumiwa au kuondolewa katika Kristo ambaye hakuwa mwenye dhambi? Na haki yake Mungu ingedhihirika vipi kwa umwagikaji wa damu ya asiye hatia?

Jibu: Kwa kuwa alizaliwa katika ukoo wa Adamu uliolaaniwa Kristo alishiriki hali yao ya unyonge kwa hivyo kazi yake ilidhihirisha hukumu iliyompasa binadamu. Ilimpendeza Mungu kufanya hivi kabla ya kumtaka binadamu kupata upatanisho na Mungu kupitia kwa mateso ya mtu huyu.

Thibitisho: "Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilishi,…" (Waebrania 2:14). "…kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake" (Waebrania 9:26). "…yaani, habari za Mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili,…" (Warumi 1:3). "…tukijua ya kuwa Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena. Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu" (Warumi 6:9-10).

56. Ni tofauti gani iliyopo kati ya Yesu na binadamu wengine juu ya jambo hili?

Jibu: Yesu akawa tofauti na watu wengine katika hali yake ile ya kutokuwa na ila kama watu wengine jambo ambalo lilimpendeza Mungu kweli kweli. Yesu hakuhitaji kutubia au kusamehewa dhambi. Haya ndiyo yalimfungulia mlango wa ufufuo. Kama angekuwa mwenye dhambi kama watu wengine basi mauti ingekuwa na nguvu juu yake. Lakini Mungu alimfufua toka kwa wafu baada ya mateso yake, na akishafufuka toka kwa wafu "mauti haya nguvu juu yake. Sasa anaishi kuwa mpatanishi wetu milele, na anaweza kuwadkoa wale wote wanaomwendea Mungu kwa Yeye." Kwa njia amekuwa haki yake Mungu kwa ajili yetu.

Thibitisho: "Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;…" (Waebrania 7:26). "Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi" (Waebrania 4:15). "Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki? (Yohana 8:46). "…na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye" (Mathayo 3:17). "Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake" (1 Yonana 3:5). "…ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao. Maana Daudi ataja habari zake, nalimwona Bwana mbele yangu sikuzote, kwa kuwa yuko upande wa mkono wangu wa kuume, nisitikisike. Kwa hiyo moyo wangu ukapendezewa, ulimi wangu ukafurahi; tena mwili wangu nao utakaa katika matumaini. Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu; wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu" (Matendo 2:24-27).

57. Tunaweza kuelewa nini maneno haya ya Paulo ati Kristo alikufa ili kuondoa dhambi (tazama swali la 55) - kwa njia ya mauti yake aweze kuangamiza kile kilichokuwa na uwezo wa mauti - yaani ibilisi. Na ibilisi ni nani?

Jibu: Ibilisi au Shetani ni neno la Biblia lililo na maana ya Dhambi katika sura zake mbali mbali. Kristo aliondolea mbali mauti kwa mateso yaliyomsibu. Dhambi ni nguvu za mauti. Hakuna kitu kama 'kiumbe shetani. Shetani wa imani za kimapokeo imetokana na kutoelewa lugha ya mafumbo ya Biblia (fumbo mfumbie mjinga). Shetani wa Biblia ana sura mbali mbali lakini inalenga unyonge wa mwili kutotii amri za Mungu. Hujitokeza katika tamaa zetu wenyewe na katika wale wanaotafuta njia zao wenyewe. Sura yake kamili, anajitokeza katika mlengo wa kisiasa wa mataifa yote.

Thibitisho: "Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,…" (Waebrania 2:14). "…kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa khabihu ya nafsi yake" (Waebrania 9:26). "Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali katama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu" (Warumi 6:23). "Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti" (Yakobo 1:14-15). "Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia" (Yakobo 4:7). "Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi;…" (Waebrania 12:4). "Na baada ya hilo tonge Shetani alimwingia. Basi Yesu akamwambia, Uyatendayo yatende upesi" (Yohana 13:27). "Yesu akawajibu, Je! mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, na mmoja wenu ni shetani?" (Yohana 6:70). "Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya. Vijana wakaondoka, wakamtia katika sanda, wakamchukua nje, wakamzika. Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea. Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo. Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe" (Matendo 5:3-9). "…ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;…" (Waefeso 2:2). "Basi napenda wajane, ambao si wazee, waolewe, wazae watoto, watawale na madaraka ya nyumbani; ili wasimpe adui nafasi ya kulaumu. Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani" ( 1 Timotheo 5:14-15). "Katika hao wamo Himenayo na Iskanda, ambao nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu" (1 Timotheo 1:20). "Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu" (Mathayo 16:23). "Akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akasema, Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu" (Marko 8:33). "Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake" (Luka 4:8). "Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia" (1 Wathesalonike 2:18). "Na kwa malaika wa kanisa lilioko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili. Napajua ukaapo, adipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani" (Ufunuo 2: 12-13). "Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilishi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze: (1 Petro 5:8). "Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima" (Ufunuo 2:10). "Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. [Amina.]" (Warumi 16:20). "Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba" (Ufunuo 12:3). "Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari" (Ufunuo 12:17). "Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo" (Ufunuo 17:9). "Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama" (Ufunuo 17:12). "Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;…" (Ufunuo 20:2).

KUHUSU NJIA YA WOKOVU

58. Je, bila Kristo twaweza kuokolewa?

Jibu: La. Mungu ametuonyesha njia hii pekee kwa wokovu, kupitia kwa binadamu Yesu Kristo.

Thibitisho: Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo" (Matendo 4:12). "Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi" (Yohana14:6). "Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu" (Yohana 8:24). "Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu" (Yohana 6:53). "Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi; akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote" Yohana 15:5). "…kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani" (Waefeso 2:12).

59. Ni kwa njia gani tunashirikishwa katika mpango huu wa wokovu katika Kristo?

Jibu: Ni katika kuuamini mpango huu. Imani yetu yahesabiwa kuwa haki.

Thibitisho: "Maana maandiko yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki" Warumi 4:3). "…bali na kwa ajili yetu sisi tutakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu;…" (Warumi 4:24). "Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo" (Warumi 5:1). "…ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti;" (Warumi 3:22).

60. Je, imani pekee yake yatosha kutuletea wokovu?

Jibu: Haitoshi. Imani lazima iambatane na utii au matendo.

Thibitisho: "Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai? Je! baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu? Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale" (Yakobo 2:20-22). "Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni" (Mathayo 7:21). "Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake" (Mathayo 16:27). "…nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake" (Ufunuo 2:23). "…na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa dahari" (Mathayo 28:20).

61. Ni matendo gani au yapi yapaswayo kutendwa na waumini?

Jibu: Kuna mambo wanayopaswa kutenda. Kwanza, wanahitajika kubatizwa.

Thibitisho: "Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha" (Matendo 10:48). "Basi sasa, unakawilia nini? Simama, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina lake" (Matendo 22:16). "Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu" (Matendo 2:38). "Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa" (Marko 16:16).

62. Ubatizo ni nini?

Jibu: Ni kuzikwa ndani ya maji.

Thibitisho: "Ni nani awezaye kukataza maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi?" (Matendo 10:47). "Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima" (Warumi 6:4). "Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu" (Wakolosai 2:12). "Kwa maana kama tulivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika tutaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;…"(Warumi 6:5).

63. Ubatizo una maana gani?

Jibu: Ni kitendo ambacho Mungu ameagiza kitendwe ili aaminiye amvae Kristo na kupata ondoleo la dhambi.

Thibitisho: "Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo" (Wagalatia 3:27). "Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?" (Warumi 6:3). "Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu" (Matendo 2:38). "Basi sasa, unakawilia nini? Simama, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina lake" (Matendo 22:16). "Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo" (1 Petro 3:21).

KUHUSU AMRI ZA KRISTO

64. Ni amri gani zingine alizoziamuru Yesu tuzifuate?

Jibu: Ametuagiza tukutanike sote kila siku ya kwanza ya juma kuumega mkate na kunywa divai kwa ukumbusho wake.

Thibitisho: "Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu" (1 Wakorintho 11:23-25). "Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane" (Matendo 20:7). "…wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia" (Waebrania 10:25). "Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;…" (1 Wakorintho 16:2).

65. Je, kuna amri zingine tunazopaswa kuzifuata na kuzitii?

Jibu: Ndio, nyingi sana. Amri zingine zatutaka tutende mambo fulani, na zingine zatushauri kutotenda mambo fulani.

66. Kariri mambo fulani tunayopaswa kuyatenda.

Jibu: (1) Tumpende Mungu na Kristo. (2) Kuwatendea wanadamu kama tunavyotaka watutendee. (3) Kupendana. (4) Kushiriki furaha na huzuni ya wenzetu. (5) Kuwapenda hata adui zetu, kuwabariki wanaotulaani, kuwatendea mema wanaotuchukia, na kuwaombea wale wanaotunyanyasa. (6) Tunapaswa kuwa tayari kwa lo lote lililo jema, kuwakopesha wahitaji, kuwasaidia watesekao. (7) Kuwa waaminifu hata kwa mabwana waovu. (8) Kuomba kila mara na kutoa shukrani kwa kila jambo. (9) Kunena ukweli kila mara. (10) Tusiwe waovu, tusiwe na lawama. (11) Tuwe wapole, na wenye ujasiri, wangwana na adili. (12) Kufuata yote yaliyo kweli, safi, yasiyo na unafiki, yenye heri na yenye sifa njema.

Thibitisho: (1) Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote" (Mathayo 22:37). "Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako" (Luka 10:27). (2) "Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii" (Mathayo 7:12). (3) "Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo" (Yohana 13:34). (4) "Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao" (Warumi 12:15). (5) "Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi, wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi" (Luka 6:27-28). "…watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubaridi; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka" (1 Petro 3:9). "…lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi;" (Mathayo 5:44). (6) "Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema;…" (Tito 3:1). "Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo" (Mathayo 5:42). "…kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni, mkijitahidi" (Warumi 12:13). (7) "Wo wote walio chini ya kongwa, hali ya utumwa, na wawahesabie bwana zao kuwa wamestahili heshima yote, jina la Mungu lisitukanwe wala mafundisho yetu. Na wale walio na bwana waaminio wasiwadharau kwa kuwa ni ndugu; bali afadhali wawatumikie, kwa sababu hao waishirikio faida ya kazi yao wamekuwa wenye imani na kupendwa. Mambo hayo uyafundishe na kuonya" (1 Timotheo 6:1,2). (8) "Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa" (Luka 18:1). "…na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;…" (Waefeso 5:1). (9) "Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake" (Waefeso 4:25). (10) "…mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,…" (Wafilipi 2:15). (11) "Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa. Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo. Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu, …" (Luka 14: 11-13). "Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini" (Wafilipi 4:4). "Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu. Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo; ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, kwamba twakesha au kwamba twalala" (1 Wathesalonike 5:8-10). (12) "Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo" (Wafilipi 4:8).

67. Hebu yataje mambo ambayo hatupaswi kuyatenda.

Jebu: (1) Tusiwe mabwana wakubwa na tusiwe na majivuno. (2) Tusilipize maovu kwa maovu. (3) Tusilipize kisasi bali tujiepusha na hasira, na tukubali kuporwa. (4) Tusitoa ili kujionyesha, mkono wetu wa kushoto usijue ufanyalo wa kiume. (5) Tusisumbukie utajiri au kuupenda ulimwengu. (6) Tusilaani tunapolaaniwa, au kutukana tunapotukanwa, lakini kinyume cha haya, tubariki. (7) Tusifanye kinyongo, tusihukumu, tusilalamike wala kulaani. (8) Tusikasirike ovyo, tusiwe na chuki au roho mbaya. (9) Tusiupende ulimwengu, tusitamani makuu au ukubwa. (10) Tusiwe wavivu katika kulipa madeni yetu. (11) Tusisengenye au kuzungumzia dhambi za watu wengine mpaka tuwe tumezungumza nao kwanza. (12) Tusiwe washiriki wa kuzini au zinaa,uasherati, uchafu, ulevi, tamaa mbaya, upinzani, chuki, unafiki, ufisadi, kuonea kijicho, na kujitakia makuu, au mazungumzo yasiyo na maana.

Thibitisho: "Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu" (Mathayo 23:11). "Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo. Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo. Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka. Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda" (Yohana 13: 13-17). (2) "Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote" (Warumi 12:17). (3) "Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana, imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake" (Warumi 12: 19-20). (4) "Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi" (Mathayo 6:1-4). (5) "…ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo" (1 Timotheo 6:8). (6) "…watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka" (1 Petro 3:9). (7) "Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu" (Yakobo 4:11). "Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi" (Mathayo 7:1). "Yatendeni mambo yote pasipo manung'uniko wala mashindano,…"(Wafilipi 2:14). (8) "Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;…" (Waefeso 4:31). "Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote" (1 Petro 2:1). (9) "Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu" (Warumi 12:2). "Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili" (Warumi 12:16). (10) "Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima. Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria" (Warumi 13:7-8). (11) "Akamgusa mkono, homa ikamwacha; naye akaondoka, akawatumikia" (Mathayo 8:15). "Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza; jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi" (Yakobo 5:19-20). (12) "Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wala kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru" (Waefeso 5:3-4).

68. Je, Injili itatuokoa ikiwa hatufuati amri hizi?

Jibu: La. Imani na ubatizo wetu utakuwa hukumu yetu IKIWA tutaishi kwa kutotii amri za Kristo. Wale tu washikao amri zake ndio watakaopata baraka.

Thibitisho: "Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake" (Ufunuo 22:14). "Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;…" (Mathayo 7:26). "Maana ingekuwa heri kwao kama waingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa" (2 Petro 1:21).

69. Kuna msamaha wa dhambi kwa wale ambao wakishaukubali ukweli wa injili wameshindwa kuendelea kutii amri za Kristo?

Jibu: Ndio. Kama ingekuwa vingine hakuna kiumbe kingeokolewa. Lakini msamaha huo una masharti: ukitubu na kuziacha dhambi zako; na tukiwasamehe wengine; na msamaha huu unaupata kwa upatanishi wa Kristo. Kama hatusamehi au kama hatupatanishi, hatuna matumaini.

Thibitisho: "BWANA, kama Wewe ungehesabu maovu, ee Bwana, nani angesimama? Lakini kwako kuna msamaha, ili Wewe uogopwe" (Zaburi 130:3-4). "…bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote" (1 Yohana 1:7). "Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,…" (1 Yohana 2:1). "Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote" (1 Yohana 1:9). "Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee" (Waebrania 7:25). "Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea" (Warumi 8:34). "Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu" (Mathayo 6:15). "Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako;" (Yohana 17:9).

KUHUSU IMANI NA INJILI

70. Umesema ya kuwa imani yetu huhesabiwa kuwa haki tunapoutii ukweli kwa njia ya ubatizo. Imani ni nini?

Jibu: Ni kitendo cha nia yetu, au kuwa na uhakikisho, unaofanywa.

Thibitisho: "Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana" Waebrania (11:1). ""Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo" (Warumi 10:17). "Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu;…" (Warumi 4:20). "Maana maandiko yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki" (Warumi 4:3). "Basi je! uheri huo ni kwa hao waliotahiriwa, au kwa hao pia wasiotahiriwa? Kwa kuwa twanena ya kwamba kwake Ibrahimu imani yake ilihesabiwa kuwa ni haki" (Warumi 4:9).

71. Ni kitu tunachopaswa kuamini au kuwa na uhakika nacho kabla ya ubatizo?

Jibu: Katika injili.

Thibitisho: "Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa" (Marko 16:16). "Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia" (Warumi 1:16). "Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa" (1 Wakorintho 1:21).

72. Injili ni nini?

Jibu: Neno Injili ina maana habari njema; na habari njema zilizofunuliwa na Yesu na Mitume ni mambo yanayohusu Ufalme wa Mungu na Jina la Yesu Kristo.

Thibitisho: "Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye,…" (Luka 8:1). "Akawaambia, Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia; maana kwa sababu hiyo nalitumwa" (Luka 4:43). "Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake" (Matendo 8:12). "Na sasa, tazameni, mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowahubiria ufalme wa Mungu, nikienda huko na huko, hamtaniona uso tena" (Matendo 20:25). "Akakaa muda wa miaka miwili mizima katika nyumba yake aliyokuwa ameipanga, akawakaribisha watu wote waliokuwa wakimwendea,…" (Matendo 28:30).

KUHUSU UFALME WA MUNGU

73. Ufalme wa Mungu ni nini?

Jibu: Ni ufalme ambao Mungu atauimarisha duniani utakaoangamiza falme zote ziliopo na kusimama imara.

Thibitisho: "Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele" (Danieli 2:44). "…nami nitakipindua kiti cha enzi cha falme, nami nitaziharibu nguvu za falme za mataifa; nami nitayapindua magari, na hao wapandao ndani yake; farasi na hao wawapandao wataanguka chini; kila mtu kwa upanga wa ndugu yake" (Hagai 2:22) "Nikaona katika njozi za usiku, na tazama,mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na uflame, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo haitapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa" (Danieli 7:13-14). "Naye BWANA atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo BWANA atakuwa mmoja, na jina lake moja" (Zekaria 14:9). "Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele" (Ufunuo 11:15).

74. Ni nani atakayekuwa mfalme katika Ufalme wa Mungu?

Jibu: Yesu Kristo.

Thibitisho: "…na Yasoni amewakaribisha; na hawa wote wanatenda mambo yaliyo kinyume cha amri za Kaisari, wakisema na kwamba yupo mfalme mwingine aitwaye Yesu" (Matendo 17:7). "Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu" (Matendo 17:31). "Nami nitamfanya yeye aliyechechemea kuwa mabaki, na yeye aliyetupwa mbali kuwa taifa lenye nguvu; na BWANA atawamiliki katika mlima Sayuni tangu sasa na hata milele" (Mika 4:7). "Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa uflame wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele" (Ufunuo 11:15). "Nami nimemweka mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu" (Zaburi 2:6).

75. Kristo atatawala peke yake katika ufalme wa Mungu au atakuwa na wasaidizi?

Jibu: Wengine watamsaidia.

Thibitisho: "…Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi;…" (2 Timotheo 2:12). "…ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi…" (Ufunuo 5:10). "Tazama, mfalme atamiliki kwa haki, na wakuu watatawala kwa hukumu" (Isaya 32:1). "Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;" (Mathayo 25:34).

76. Ni nani hao watakaotawala pamoja na Kristo katika ufalme wa Mungu?

Jibu: Watakatifu.

Thibitisho: "…hata akaja huyo mzee wa siku, nao watakatifu wake Aliye juu wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme" (Danieli 7:22). "Lakini watakatifu wake Aliye juu wataupokea ufalme, na kuumiliki huo ufalme milele, naam hata milele na milele" (Danieli 7:18). "Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo?" (1 Wakorintho 6:2). "Ili kufanya kisasi juu ya mataifa, na adhabu juu ya kabila za watu. Wawafunge wafalme wao kwa minyororo, na wakuu wao kwa pingu za chuma. Kuwafanyia hukumu iliyoandikwa; hiyo ndiyo heshima ya watauwa wake wote. Haleluya" (Zaburi 149:7-9).

77. Watakatifu au watauwa ni akina nani?

Jibu: Wale Wanaoamini na kutii injili.

Thibitisho: "…kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu. Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo" (Warumi 1:7). "…kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu" (1 Wakorintho 1:2). "…aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, ili kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo" (2 Wathesalonike 2:14). "Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu; kwa watakatifu walioko wanaomwamini Kristo Yesu" (Waefeso 1:1). "Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu" (Waefeso 1:13).

78. Mungu aliwahi kuwa na ufalme duniani awali?

Jibu: Ndio, ufalme wa Israeli ulikuwa ufalme wa Mungu.

Thibitisho: "Maana ufalme una BWANA, naye ndiye awatawalaye mataifa" (Zaburi 22:28). "Haleluya. Israeli alipotoka Misri, na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni. Yuda ilikuwa patakatifu pake, Israeli milki yake" (Zaburi 114:1-2). "Hata sasa mwajidhania kuwa mtauzuia ufalme wa BWANA mikononi mwa wana wa Daudi; nanyi mmekuwa jamii kubwa, na kwenu mna ndama za dhahabu alizowafanyia Yeroboamu kuwa miungu" (2 Mambo Ya Nyakati 13:8). "Ndipo Sulemani akaketi katika kiti cha enzi cha BWANA, awe mfalme badala ya Daudi babaye, akafanikiwa; nao Israeli wote wakamtii" (1 Mambo Ya Nyakati 29:23).

79. Je, ufalme wa Mungu, utakaotawaliwa na Kristo na watakatifu, utakuwa na uhusiano wowote na ule wa Israeli uliokuwepo awali?

Jibu: Ufalme wa Mungu, utakaotawaliwa na Kristo pamoja na watakatifu, utakuwa ni ufalme wa Israeli uliorejeshwa.

Thibitisho: "Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?" (Matendo 1:6). "…nami nitarejeza upya waamuzi wako kama walivyokuwa hapo kwanza, na washauri wako kama hapo mwanzo; baada ya hayo utaitwa, Mji wa haki, mji mwaminifu" (Isaya 1:26). "Siku hiyo nitaiinua tena maskani ya Daudi iliyoanguka, na kuziba mahali palipobomoka; nami nitayainua magofu yake, na kuyajenga kama siku za kale;…" (Amosi 9:11). "Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli" (Mathayo 19:28).

80. Ufalme wa Israel uliorejeshwa utachukua nafasi ya ardhi ya hapo awali?

Jibu: Ndio. Utaimarishwa katika nchi ile ile iliyotawaliwa na Daudi, nchi ambayo damu ya masihi ilimwagika kwayo.

Thibitisho: "Nchi iliyokuwa ukiwa italimwa, ijapokuwa ilikuwa ukiwa mbele ya macho ya watu wote waliopita" (Ezekieli 36:34). "Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefsiba; na nchi yako Beula; kwa kuwa BWANA anakufurahia, na nchi yako itaolewa" (Isaya 62:4). "Na kwa kuwa umeachwa na kuchukiwa, hata ikawa hapana mtu aliyepita ndani yako, nitakufanya kuwa fahari ya milele, furaha ya vizazi vingi" (Isaya 60:15). "Nao watajenga mahali pa kale palipoharibiwa, watapainua mahali palipokuwa ukiwa zamani, watatengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa kizazi baada ya kizazi" (Isaya 61:4). "Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza" (Zekaria 12:10). "Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa BWANA, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA litatoka Yerusalemu" (Mika 4:2).

81. Je, ufalme huo utakuwa wa taifa lile lile la awali, yaani, Wayahudi ambao sasa wametawanyika?

Jibu: Ndio, Wayahudi, uzao wa Ibrahimu waliotawanyika kwa sasa, katika mataifa yote ya ulimwengu, watakusanywa tena katika nchi yao wenyewe, na wafanywe taifa tukufu na lenye haki.

Thibitisho: "Naye atawatwekea mataifa bendera, atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za dunia" (Isaya 11:12). "Lisikieni neno la BWANA, enyi mataifa, litangazeni visiwani mbali; mkaseme, Aliyemtawanya Israeli atamkusanya, na kumlinda, kama mchungaji alindavyo kundi lake" (Yeremia 31:10). "BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawaokoa watu wangu toka nchi ya mashariki, na toka nchi ya magharibi;" (Zekaria 8:7). "Ukawaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitawatwaa wana wa Israeli toka kati ya mataifa walikokwenda, nami nitawakusanya pande zote, na kuwaleta katika nchi yao wenyewe; nami nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi hiyo, juu ya milima ya Israeli; na mfalme mmoja atakuwa mfalme wao wote; wala hawatakuwa tena mataifa mawili, wala hawatagawanyikana kuwa falme mbili tena, hata milele" (Ezekieli 37:21-22).

KUHUSU IBRAHIMU, ISAKA NA YAKOBO

82. Ibrahimu alikuwa nani?

Jibu: Mwanzoni alikuwa mkazi wa Mesopotamia, upande wa mashariki wa mto frati. Lakini alipokuwa na umri wa miaka 75, aliwaacha marafiki zake na kuhamia Kanani.

Thibitisho: "Nami nikamtwaa Ibrahimu baba yenu toka ng'ambo ya Mto, nikamwongoza katika nchi yote ya Kanaani; nikaongeza uzao wake, nikampa Isaka" (Yoshua 24:3). "Wewe ndiwe BWANA, Mungu, uliyemchagua Abramu, na kumtoa katika Uri wa Wakaldayo, na kumpa jina la Ibrahimu;" (Nehemia 9:7). "Ndipo alipotoka katika nchi ya Wakaldayo, akakaa Harani, akatoka huko baada ya kufa babaye, Mungu akamhamisha mpaka nchi hii mnayokaa ninyi sasa" (Matendo 7:4).

83. Kwa nini Ibrahimu alihamia Kanani?

Jibu: Kwa sababu Mungu alimwamuru afanye vile.

Thibitisho: "Naye akasema, Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni: Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Ibrahimu, alipokuwa katika Mesopotamia, kabla hajakaa Harani, akamwambia, Toka katika nchi yako na katika jamaa zako, ukaende hata nchi nitakayokuonyesha" (Matendo 7:2-3). "BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;…" (Mwanzo 12:1).

84. Kwa nini Mungu alimwamuru Ibrahimu kuhamia Kanani?

Jibu: Kwa sababu ya mpango aliokuwa nao kwa Ibrahimu kumhusu yeye na ulimwengu mzima.

Thibitisho: "Mwangalieni Ibrahimu, baba yenu, na Sara, aliyewazaa; kwa maana alipokuwa mmoja tu nalimwita, nikambariki, nikamfanya kuwa wengi. Maana BWANA ameufariji Sayuni; amepafariji mahali pake palipokuwa ukiwa; amefanya jangwa lake kuwa kama bustani ya Adeni, na nyika yake kama bustani ya BWANA; furaha na kicheko zitaonekana ndani yake, kushukuru, na sauti ya kuimba. Nisikilizeni mimi, enyi watu wangu; nisikieni, taifa langu; maana sheria itatoka kwangu, nami nitaistarehesha hukumu yangu iwe nuru ya mataifa" (Isaya 51:2-5). "…watu wale niliojiumbia nafsi yangu, ili wazitangaze sifa zangu"(Isaya 43:21). "Nawe, Israeli, mtumishi wangu; Yakobo, niliyekuchagua; mzao wa Ibrahimu, rafiki yangu;…"(Isaya 41:8).

85. Mungu alikuwa na nia au mpango gani kwa Ibrahimu?

Jibu: Kumfanya Ibrahimu kuwa taifa kubwa kwa utukufu wa Mungu na kumbariki mwanadamu hatimaye.

Thibitisho: "…nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa: (Mwanzo 12:2-3). "…lakini hakika yangu, kama niishivyo, tena kama dunia hii nzima itakavyojawa na utukufu wa BWANA;" (Hesabu 14:21). "Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa" (Isaya 45:23).

86. Mungu alimfunulia mtu mwingine yeyote mpango huu wake?

Jibu: Ndio, kwa mwanawe Ibrahimu, Isaka, na kwa mwanawe Isaka, Yakobo.

Thibitisho: "Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia" (Mwanzo 26:4). "Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa" (Mwanzo 28:14). "Agano alilofanya na Ibrahimu, na uapo wake kwa Isaka" (Zaburi 105:9). "Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile" (Waebrania 11:8-9).

87. Mungu aliweka msingi wa kazi yake vipi na Ibrahimu, Isaka na Yakobo?

Jibu: Alifanyiza agano nao wa kuwapa nchi ya Kanani, nchi walimokaa kama wageni, ili iwe maskani yao milele.

Thibitisho: "…maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele" (Mwanzo 13:15). "Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,…" (Mwanzo 15:18). "Alilomthibitishia Yakobo liwe amri, na Israeli liwe agano la milele. Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani, iwe urithi wenu mliopimiwa" (Zaburi 105:10-11). "BWANA akamtokea, akasema, Usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia. Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako. Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia" (Mwanzo 26:2-4). "Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa" (Mwanzo 28:13-14).

88. Je, Ibrahimu, Isaka na Yakobo walipata kumiliki nchi hiyo ya ahadi ya Kanani?

Jibu: La. Walikuwa wageni katika nchi hiyo ya ahadi muda wote wa uhai Wao na kufa (wakazikwa huko Hebroni pasipo kuimiliki nchi hiyo).

Thibitisho: "Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi. Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe. Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea. Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji" (Waebrania 11:13-15). "Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi; kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi" (Waebrania 11:39-40). "Wala hakumpa urithi humu hata kiasi cha kuweka mguu; akaahidi kwamba atampa, iwe milki yake, na ya uzao wake baadaye alipokuwa hana mtoto" (Matendo 7:5). "Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile" (Waebrania 11:8-9).

89. Je, Mungu ataitimiza ahadi yake kwa Ibrahimu, Isaka na Yakobo kwa kuwapa nchi ya Kanani nchi walimokaa kama wageni siku za uhai wao?

Jibu: Mungu kwa uhakika atatimiza ahadi yake. Atawafufua Ibrahimu, Isaka na Yakobo na kuwapa miliki ya nchi hiyo wakati ambapo ufalme wa Mungu utakuwa umeimarishwa huko. Itakuwa nchi nzuri mfano wa mbinguni.

Thibitisho: "Wewe utamtimilizia Yakobo kweli yako, na Ibrahimu rehema zako, ulizowaapia baba zetu tangu siku za kale" (Mika 7:20). "Na kwa habari ya wafu ya kwamba wafufuliwa, hamjasoma katika kitabu cha Musa, Sura ya Kijiti, jinsi Mungu alivyomwambia, akisema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?" (Marko 12:26). "Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje" (Luka 13:28). "Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;…" (Mathayo 8:11). "Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji" (Waebrania 11:16).

KUHUSU UKOMBOZI WA ISRAELI KUTOKA MISRI

90. Akisha kuweka imara agano lake na Ibrahimu, Isaka na Yakobo Mungu alifanya matayarisho yapi ili kuutekeleza mpango wake?

Jibu: Alipeleka familia ya Yakobo katika nchi ya Misri ambako waliongezeka idadi yao baada ya kitambo cha kuwa huko na wakafanywa watumwa na Farao aliyetumikisha kwa kuwafanya wachomaji matofali.

Thibitisho: Mwanzo 35-Mwanzo 50; Kutoka 1, 2.

91. Walikaa muda gani Misri?

Jibu: Kati ya miaka 200 na 300.

Thibitisho: "Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana haujatimia uovu wa Waamori bado" (Mwanzo 15:16). "Nisemalo ni hili; agano liliothibitishwa kwanza na Mungu, torati iliyotokea miaka mia nne na thelathini baadaye hailitangui, hata kuibatilisha ile ahadi" (Wagalatia 3:17).

92. Waliondokaje Misri?

Jibu: Mungu alimtuma Musa kumwendea Farao akiwa na ujumbe wa kutaka waachiliwe huru. Na Farao alipodinda kuwaachilia, Mungu alipeleka mapigo (tauni) katika nchi hiyo, moja baada ya nyingine kufikia mapigo kumi. Na baada ya hayo Farao aliwapa rukhusa ya kugura.

Thibitisho: Mwanzo 3-14.

93. Je, walienda moja kwa moja hadi katika nchi ya ahadi?

Jibu: La. Mungu aliwaeleza upande wa magharibi wa bahari ya Shamu, walikokumbana na hatari kuu; kwani Farao aliposikia ya kuwa wako kule ambako hawangeweza kuepuka. Aliwaandama akiwa na kikosi kikubwa cha askari ili awakamate na kuwarejesha Misri.

Thibitisho: Kutoka 14.

94. Mungu alifanya nini ili awaachilie watu wake kutoka kwa nuksi waliokuwamo?

Jibu: Aliwafunulia njia katika bahari ili Waisraeli wakaitumie kuvukia. Waisraeli walifika ng'ambo salama, na Wamisri walipowafuatia Mungu aliwafunika kwa bahari wakazama maji.

Thibitisho: Kutoka 14.

95. Ni kwa sababu gani Mungu alifanyiza miujiza hii yote?

Jibu: Ili apate kudhihirisha kuwepo kwake na nguvu zake kwa Waisraeli na dunia nzima.

Thibitisho: "Au Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia taifa toka kati ya taifa lingine, kwa majaribu, na kwa ishara, na kwa maajabu, na kwa vita, na kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa maogofya makuu, kama vile BWANA, Mungu wenu, alivyowatendea ninyi katika Misri, mbele ya macho yenu? Wewe umeonyeshwa haya, ili upate kujua ya kuwa BWANA ndiye Mungu, hapana mwingine ila yeye" (Kumbukumbu La Torati 4:34-35). "Lakini akawaokoa kwa ajili ya jina lake, ayadhihirishe matendo yake makuu" (Zaburi 106:8). "…katika siku ile naliwainulia mkono wangu, kuwatoa katika nchi ya Misri, na kuwaingiza katika nchi niliyowapelelezea, ijaayo maziwa na asali; ambayo ni utukufu wa nchi zote; nikawaambia, Kila mtu kwenu na atupilie mbali machukizo ya macho yake, wala msijitie unajisi kwa vinyago vya Misri; Mimi ni BWANA, Mungu wenu. Lakini waliniasi, wala hawakutaka kunisikiliza; hawakutupilia mbali kila mtu machukizo ya macho yake, wala hawakuviacha vinyago vya Misri; ndipo nikasema kwamba nitamwaga ghadhabu yangu juu yao, ili kuitimiza hasira yangu juu yao, katikati ya nchi ya Misri. Lakini nalitenda kwa ajili ya jina langu, ili lisitiwe unajisi mbele ya macho ya mataifa, ambao walikaa pamoja nao, ambao machoni pao nalijidhihirisha kwao, kwa kuwatoa katika nchi ya Misri" (Ezekieli 20:6-9). "BWANA akamwambia Musa, Ingia wewe kwa Farao; kwa kuwa mimi nimeufanya moyo wake mzito, nipate kuzionyesha ishara zangu hizi kati yao; nawe upate kusema masikioni mwa mwanao, na masikioni mwa mjukuu wako, ni mambo gani niliyotenda juu ya Misri, na ishara zangu nilizozifanya kati yao; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA" (Kutoka 10:1-2). "…lakini, nilikusimamisha wewe kwa sababu ii hii, ili nikuonyeshe uweza wangu, tena kwamba jina langu litangazwe katika dunia yote" (Kutoka 9:16). "Nami siku hiyo nitatenga nchi ya Gosheni, watu wangu wanayokaa, ili hao mainzi wasiwe huko; ili kwamba upate kujua wewe ya kuwa mimi ndimi BWANA kati ya dunia" (Kutoka 8:22).

96. Wasraeli walipokuwa wamevuka bahari ya Shamu Mungu aliwafanyia jambo gani lingine?

Jibu: Aliwaongoza hadi jangwani, Sinai, Kwenye malima na mabonde makuu na akawaonyesha kuwepo kwake waziwazi kwa kuteremka na kuwa juu ya mlima wa Sinai kati ya ukungu na mawingu yaliyoufunika mlima na kuwazungumzia kwa sauti kuu na wote wakamsikia.

Thibitisho: "BWANA akaushukia mlima, juu ya kilele cha mlima; BWANA akamwita Musa aende hata kilele cha mlima; Musa akapanda juu" (Kutoka 19:20). "…siku ile uliyosimama mbele za BWANA wako huko Horebu, BAWANA aliponiambia, Nikusanyieni watu hawa, nami nitawasikizisha maneno yangu, ili wajifunze kunicha mimi siku zote watakazoishi duniani, wakapate na kuwafundisha watoto wao. Mkakaribia, mkasimama chini ya ule mlima; mlima ukawaka moto mpaka kati ya mbinguni, kwa giza na mawingu, na giza kuu. BWANA akasema nanyi kutoka kati ya moto; mkasikia sauti ya maneno, lakini hamkuona umbo lo lote; sauti tu. Akawahubiri agano lake, alilowaamuru kulitenda, yaani, zile amri kumi; akaziandika juu ya mbao mbili za mawe. BWANA akaniamuru wakati ule niwafundishe maagizo na hukumu, mpate kuzitenda katika nchi ile mtakayoivukia ili kuimiliki" (Kumbukumbu La Torati 4:10-14). "BWANA alisema nanyi uso kwa uso mlimani, toka kati ya moto;…" (Kumbukumbu La Torati 5:4).

97. Kwa nini alifanya hivyo?

Jibu: Ili watu wapate kumwamini Musa kama nabii wa Mungu, na wawe tayari kutii sheria ambayo angewapa.

Thibitisho: "BWANA akamwambia Musa, Tazama, mimi naja kwako katika wingu zito ili watu hawa wasikie nitakaposema nawe, nao wapate kukuamini wewe nawe hata milele. Musa akamwambia BWANA hayo maneno ya watu" (Kutoka 19:9). "…siku ile uliyosimama mbele za BWANA wako huko Horebu, BWANA aliponiambia, Nikusanyieni watu hawa, nami nitawasikizisha maneno yangu, ili wajifunze kunicha mimi siku zote watakazoishi duniani, wakapate na kuwafundisha watoto wao" (Kumbukumbu La Torati 4:10).

98. Mungu aliwambia Waisraeli nini?

Jibu: Aliwapa amri kumi.

Thibitisho: "BWANA akasema nanyi kutoka kati ya moto; mkasikia sauti ya maneno, lakini hamkuona umbo lo lote; sauti tu. Akawahubiri agano lake, alilowaamuru kulitenda, yaani, zile amri kumi; akaziandika juu ya mbao mbili za mawe" (Kumbukumbu La Torati 4:12-13).

99. Aliwapa sheria nyingine zaidi ya amri zile kumi?

Jibu: Ndio. Alimwambia Musa mambo mengine mengi, mambo ambayo Musa aliwapasha watu.

Thibitisho: "Akawahubiri agano lake, alilowaamuru kulitenda, yaani, zile amri kumi; akaziandika juu ya mbao mbili za mawe. BWANA akaniamuru wakati ule niwafundishe maagizo na hukumu, mpate kuzitenda katika nchi ile mtakayoivukia ili kuimiliki" (Kumbukumbu La Torati 4:13-14).

KUHUSU AGANO LA KWANZA

100. Je, Mungu alifanya agano lolote na watu kuhusiana na mambo haya?

Jibu: Ndio. Mungu alikuwa tayari kuwabariki kwa neema au baraka mbalimbali ikiwa wangefuata na kutii amri walizopewa. Na watu wakaahidi kutenda yote atakayoamuru Mungu. Mungu basi akawapa sheria naye Musa akaiandika katika kitabu, na akawasomea watu. Halafu akanyunyizia kitabu na pia watu kwa damu ya dhabihu au sadaka, na kwa njia hiyo agano ikafanyika kati ya Mungu na watu.

Thibitisho: "Musa akaenda akawaambia watu maneno yote ya BWANA, na hukumu zake zote; watu wote wakajibu kwa sauti moja, wakasema, Maneno yote aliyoyanena BWANA tutayatenda. Basi Musa akayaandika maneno yote ya BWANA, akaondoka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya kabila kumi na mbili za Israeli, akapeleka vijana wa wana wa Israeli, waliotoa sadaka za kuteketezwa, wakamchinjia BWANA sadaka za amani za ng'ombe. Musa akatwaa nusu ya ile damu, akaitia katika mabakuli; na nusu ya ile damu akainyunyiza juu ya madhabahu. Kisha akakitwaa kitabu cha agano akakisoma masikioni mwa watu; wakasema, Hayo yote aliyoyanena BWANA tutayatenda, nasi tutatii. Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya BWANA pamoja nanyi katika maneno haya yote" (Kutoka 24:3-8). "Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote, akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu. Na ile hema nayo na vyombo vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivyo hivyo" (Waebrania 9:19-21).

101. Agano laitwaje katika Maandiko?

Jibu: Yaitwa ya Kwanza au Agano la Kale.

Thibitisho: "Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili. Maana, awalaumupo, asema, angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya; halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, mimi nami sikuwajali, asema Bwana. Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli baada ya siku zile, asema Bwana; nitawapa sheria zangu katika nia zao, na katika mioyo yao nitaziandika; nami nitakuwa Mungu kwao, nao watakuwa watu wangu. Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; kwa maana wote watanijua, tangu mdogo wao hata mkubwa wao. Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, na dhambi zao sitazikumbuka tena. Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka" (Waebrania 8:7-13).

102. Kwa nini yaitwa ya Kwanza au Agano la Kale, hali kulikuwepo na agano hapo awali kwa Ibrahimu-Swali la 86.

Jibu: Kwa sababu, ingawa Agano linalohusu sheria ya Musa ni ya mwisho kutolewa, ilikuwa ya kwanza kutekelezwa, na ilikuwa sheria iliyotumiwa na Waisraeli katika maisha yao ya kawaida kama taifa kwa miaka mingi kabla ya kuthibitishwa kwa Agano na Ibrahimu kwa umwagikaji wa damu ya masihi.

Thibitisho: "Nisemalo ni hili; agano lililothibitishwa kwanza na Mungu, torati iliyotokea miaka mia nne na thelathini baadaye hailitangui, hata kuibatilisha ile ahadi. Kwa maana urithi ukiwa kwa sheria, hauwi tena kwa ahadi; lakini Mungu alimkirimia Ibrahimu kwa njia ya ahadi. Torati ni nini basi? Iliingizwa kwa sababu ya makosa, hata aje huyo mzao aliyepewa ile ahadi; iliamriwa kwa utumishi wa malaika kwa mkono wa mjumbe" (Wagalatia 3:17-19). "Kwa maana nasema, ya kwamba Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu;…"(Warumi 15:8). "Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu" (Luka 22:20). "naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu. Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo" (1 Wakorintho 11:24-26).

KUHUSU WAISRAELI KATIKA JANGWA

103. Kitu gani kilitendeka baada ya Waisraeli kupewa sheria, na kuimarishwa kwa mambo yote yaliyoambatana na sheria hiyo?

Jibu: Mungu aliwaamuru Waisraeli waende na kutwa nchi ya Kanani na wawaangamize mataifa, inenyeji wa nchi hiyo.

Thibitisho: Hesabu 13:1-20. "Tukasafiri kutoka Horebu, tukapita katikati ya jangwa lile kubwa la kutisha mliloliona, njia ile ya kuiendea nchi ya vilima vya Waamori, kama BWANA, Mungu wetu, alivyotuamuru, tukafika Kadesh-barnea. Nami nikawaambia, Mmefika nchi ya vilima ya Waamori, anayotupa sisi BWANA, Mungu wetu. Tazama, BWANA, Mungu wako, ameiweka nchi mbele yako; haya panda, itamalaki, kama BWANA, Mungu wa baba zako, alivyokuambia; usigope wala usifadhaike" (Kumbukumbu La Torati 1:19-21).

104. Walifanya kama walivyoamuriwa?

Jibu: Walitaka kufanya hivyo, lakini waliposikia kuwa mataifa ya Kanani yalikuwa na nguvu, waliogopa, na wakakata shauri kutoendelea mbele, lakini kumwua Musa, na wamteue kiongozi mwingine, ambaye angewaongoza na kuwarejesha Misri.

Thibitisho: "Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi. Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno. Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi" (Hesabu 13:31-33). Hesabu 14:1-10. "Nanyi mkanikaribia kila mmoja wenu, mkasema, Na tupeleke watu mbele yetu, ili watupelelezee nchi na kutuletea habari za njia itupasayo kuipandia, na za miji tutakayoifikia. Neno hili likanipendeza sana; nikatwaa watu kumi na wawili, mtu mmoja wa kila kabila" (Kumbukumbu La Torati 1:22-23). "Lakini katika jambo hili hamkumwamini BWANA, Mungu wenu, aliyewatangulia njiani, usiku kwa moto, kuwaonyesha njia mtakayoiendea, na mchana kwa hilo wingu, ili apate kuwatafutia mahali pa kusimamisha hema zenu" (Kumbukumbu La Torati 1:32-33).

105. Mungu aliwafanyaje kwa huku kutotii kwao?

Jibu: Akishaonyesha uwezo wake kati ya marago ya kumwokoa Musa, aliamuru kundi lote lirudi jangwani, na wakabakia huko muda wa miaka arobaini, mpaka watu wote waliokuwa na umri wa zaidi ya miaka ishirini walipokufa.

Thibitisho: Hesabu 14:10-35. Kumbukumbu La Torati 1:34-40.

106. Ni kitu gani kilichotukia baada ya mwisho wa miaka hiyo arobaini?

Jibu: Mwisho wa miaka arobaini, Waisraeli walitokea upande wa mashariki wa mto Yordani na kuingia Kanani. Mataifa ya upande huo yakishaangamizwa Musa akaaga dunia; halafu wana wa Israeli wakauvuka mto wa Yordani, na kuwashambulia mataifa ng'ambo hii.

Thibitisho: Kumbukumbu La Torati 2-3.

107. Je, ulikuwa uovu kwa taifa la Israeli kupigana na mataifa ya Kanani?

Jibu: La. Mataifa ya Kanani yalikuwa yamekiuka mipaka ya uovu, na Mungu alikuwa amewaamuru Waisraeli kuwaadhibu. Ingekuwa ukatili na uovu kama wasingetekeleza amri hii.

Thibitisho: "Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu; (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;) ili kwamba hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu" (Mambo Ya Walawi 18:26-28). "Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye. Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA. Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko" (Mambo Ya Walawi 18:20-23). "Usiseme moyoni mwako, BWANA, Mungu wako, atakapokwisha kuwasukumia nje mbele yako, ukasema, Ni kwa haki yangu alivyonitia BWANA niimiliki nchi hii; kwani ni kwa ajili ya uovu wa mataifa haya BWANA, awafukuza nje mbele yako" (Kumbukumbu La Torati 9:4).

KUHUSU MEMA NA MAOVU

108. Uo'vu ni nini na mema ni yapi?

Jibu: Ni maovu yote anayoyakataza Mungu; anayoyaamuru Mungu yote ni mema.

Thibitisho: "Neno niwaagizalo lo lote liangalieni kulifanya; usiliongeze, wala usilipunguze" (Kumbukumbu La Torati 12:32). "Naye Samweli akasema, Je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, na kusikia kuliko mafuta ya beberu" (1Samweli 15:22). "Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi"(1 Yohana 3:4). ""Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki" (Warumi 5:19).

109. Kwa kuwa Mungu amesema, "Usiue," haikuwa uovu kuwaua Wakanani?

Jibu: La. Kwa kuwa hiyo ilikuwa amri yake Mungu. Kuna wakati wa kuua na majira ya kuwaacha watu hai. Mungu ana sababu zake, na anapotoa amri, mwanadamu hana budi kutii. Mungu anaweza kutenda apendavyo. Hakuna anayeweza kuthubutu kubishana naye.

Thibitisho: "…wakati BWANA, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao;…" (Kumbukumbu La Torati 7:2). "Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo BWANA, Mungu wako, kuwa urithi, usihifadhi kuwa hai kitu cho chote kipumzikacho;…" (Kumbukumbu La Torati 20:16). "Kwa kila jambo kuna majira yake, na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa; wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;…" (Mhubiri 3:1-3). "Wakati huo Samweli akamwambia Sauli; BWANA alinipeleka nikutie mafuta, uwe mfalme wa watu wake Israeli; basi sasa, isikilize sauti ya maneno ya BWANA. BWANA wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu mambo hayo Amaleki waliyowatenda Israeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri. Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda" (1 Samweli 15:1-3). "Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng'ombe, na vinono, na wana-kondoo, na cho chote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali cho chote kilichokuwa kibaya na kibovu, ndicho walichokiangamiza kabisa" (1 Samweli 15:9). "Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme" (1 Samweli 15:23). "Lakini Samweli akamjibu, Kama upanga wako ulivyofanya wanawake kufiwa na watoto wao, vivyo hivyo mama yako atafiwa miongoni mwa wanawake. Basi Samweli akamkata Agagi vipande mbele za BWANA huko Gilgali" (1 Samweli 15:33). "Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya BWANA kwa ulegevu; na alaaniwe auzuiaye upanga wake usimwage damu" (Yeremia 48:10). "…na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu; naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe?" (Danieli 4:35). "BWANA amefanya kila lililompendeza, katika mbingu na katika nchi, katika bahari na katika vilindi vyote" (Zaburi 135:6).

KUHUSU WAISRAELI SIKU ZA WAAMUZI

110. Waisraeli wakiwa chini ya uongozi wa Yoshua wakishauangamiza umilikaji wa wana Kanani (Wapelestina) waliifanyaje nchi?

Jibu: Waliigawa yao na kuishi kwa sheria ambazo Musa aliwapa.

Thibitisho: Yoshua 18:1-10. "Akawatoa watu wake kwa shangwe, na wateule wake kwa nyimbo za furaha. Akawapa nchi za mataifa, wakairithi kazi ya watu; ili wazishike amri zake, na kuzitii sheria zake. Haleluya" (Zaburi 105:43-45).

111. Waliendelea kuzitii sheria hizi?

Jibu: Ndio. Muda wote wa kuwepo kwake Yoshua na kizazi chake. Baadaye wakaziacha sheria hizo na kufanya sawa na Watu wa Kanani. Wakaacha kumwabudu Mungu na kugeukia miungu.

Thibitisho: Waamuzi 2:6-13. "Hawakuwaharibu watu wa nchi kama BWANA alivyowaambia; bali walijichanganya na mataifa, wakajifunza matendo yao. Wakazitumikia sanamu zao, nazo zikawa mtego kwao. Naam, walitoa wana wao na binti zao kuwa dhabihu kwa mashetani. Wakamwaga damu isiyo na hatia, damu ya wana wao na binti zao; waliowatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani; nchi ikatiwa unajisi kwa damu. Ndivyo walivyotiwa uchafu kwa kazi zao, wakafanya uasherati kwa matendo yao" (Zaburi 106:34-39).

112. Ni nini ilikuwa matokeo ya kutofuata amri za Musa?

Jibu: Mungu aliwaletea dhiki kubwa kwa kuwaachilia mataifa jirani kuwapiga na kuwachukulia nyumba zao, mali yao na mashamba yao.

Thibitisho: "Hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao. Kila walikokwenda, mkono wa BWANA ulikuwa juu yao kuwatenda mabaya, kama BWANA alivyosema, na kama BWANA alivyowaapia; nao wakafadhaika sana" (Waamuzi 2:14-15). "Hasira ya BWANA ikawaka juu ya watu wake, akauchukia urithi wake. Akawatia mikononi mwa mataifa, nao waliowachukia wakawatawala. Adui zao wakawaonea, wakatiishwa chini ya mkono wao. Mara nyingi aliwaponya, bali walikuwa wakimwasi kwa mashauri yao, wakadhilika katika uovu wao" (Zaburi 106:40-43).

113. Je, mambo haya yaliwaangamiza Waisraeli?

Jibu: La. Walipopatwa na masaibu walimlilia Mungu na kutubu dhambi zao; na kwa muda wa zaidi ya miaka mia nne wakawa chini ya Waamuzi waliowaokoa kutoka kwa masaibu mbalimbali.

Thibitisho: Waamuzi 2:16-23. "Na alipokwisha kuwaharibu mataifa saba katika nchi ya Kanaani akawapa nchi yao iwe urithi kwa muda wa miaka kama mia nne na hamsini; baada ya hayo akawapa waamuzi hata zamani za nabii Samweli" (Matendo 13:19-20).

114. Hebu taja majina ya Waamuzi aliowateua Mungu.

Jibu: Baada ya Yoshua, Othnielo, Ehudi, Debora na Baraka, Gidion, Abimeleki, Tola, Yairo, Yeftha, Ibzani, Eloni, Abdoni, Samson, Eli na Samweli. Hawa waamuzi, ingawa wanafuatana mmoja baada ya mwingine, hawakuchukua nafasi hiyo kila baada ya wa kwanza kuondoka. Kulikuwapo na wakati ambapo Waisraeli waliteseka na tesi za makabila jirani kabla ya Mwamuzi kujitokeza.

Thibitisho: Kitabu Cha Waamuzi na 1 Samweli 1-3.

KUHUSU ISRAELI KUWA FALME AU DOLA

115. Ni mabadiliko gani yaliyotokea mwisho wa mwamuzi wa mwisho?

Jibu: Waisraeli walimtamani mfalme wawe kama mataifa jirani. Walimjia Samweli na wakamsihi awape mfalme.

Thibitisho: "Hata Samweli alipokuwa mzee, aliwafanya wanawe wawe waamuzi juu ya Israeli. Na jina la mwanawe mzaliwa wa kwanza aliitwa Yoeli; na jina la wa pili Abiya; walikuwa waamuzi katika Beer-sheba. Ila wanawe hawakuenda katika njia zake, bali waliziacha, ili wapate faida; wakapokea rushwa, na kupotosha hukumu. Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama; wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote" (1 Samweli 8:1-5).

116. Je, Samweli alikubaliana na matakwa yao?

Jibu: Mungu alimwuliza Samweli afanye sawasawa na matakwa yao. Na Samweli akampa mafuta Saulo mwana wa Kishi awe mfalme wao.

Thibitisho: "Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba BWANA. BWANA akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao. Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe. Basi sasa, isikilize sauti yao; walakini, uwaonye sana, na kuwaonyesha desturi ya mfalme atakayewamiliki" (1 Samweli 8:6-9). 1 Samweli 9 na 10.

117. Je, Saulo alikuwa mfalme mwema?

Jibu: La. Mara nyingi hakuitii amri ya Mungu katika kutenda aliyoamriwa.

Thibitisho: "Naye Samweli akamwambia Sauli, Umefanya upumbavu; hukuishika amri ya BWANA, Mungu wako, aliyokuamuru; kwa maana BWANA angaliufanya ufalme wako kuwa imara juu ya Israeli milele" (1 Samweli 13:13). "Mbona, basi, hukuitii sauti ya BWANA, bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA?" (1 Samweli 15:19). "Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake alilomkosa BWANA, kwa sababu ya neno la BWANA, asilolishika; na tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake,…" (1 Mambo Ya Nyakati 10:13).

118. Matokeo ya kutotii kwake Saulo yalikuwa vipi?

Jibu: Mungu alimkatalia mbali asiwe mfalme na mahali pake akachaguliwa Daudi mwana wa Yese kuchukua mahali pake.

Thibitisho: "Naye Samweli akamwambia Sauli, Umefanya upumbavu; hukuishika amri ya BWANA, Mungu wako, aliyokuamuru; kwa maana BWANA angaliufanya ufalme wako kuwa imara juu ya Israeli milele. Lakini sasa ufalme wako hautadumu; BWANA amejitafutia mtu aupendezaye moyo wake, naye BWANA amemwamuru yeye kuwa mkuu juu ya watu wake, kwa sababu wewe hukulishika neno lile BWANA alilokuamuru" (1 Samweli 13:13-14). "Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la BWANA, BWANA naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli. Naye Samweli alipogeuka, aende zake, Sauli akaushika upindo wa vazi lake, nalo likararuka. Basi Samweli akamwambia, Leo BWANA amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe. Tena Yeye aliye Nguvu za Israeli hatanena uongo, wala hataona majuto; maana siye mwanadamu, hata ajute" (1 Samweli 15:26-29). "Samweli akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa BWANA amekuacha, naye amekuwa adui yako? Yeye BWANA amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; BWANA amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi. Kwa sababu wewe hukuitii sauti ya BWANA, wala hukumtimilizia hasira yake kali juu ya Amaleki; kwa sababu hii BWANA amekutendea hili leo" (1 Samweli 28:16-18).

119. Je, Daudi alikuwa mfalme mwema?

Jibu: Ndio. Alikuwa mwema kwani moyo wake uliambatana na Mungu. Alifanya yote ya kumpendeza muda wa uhai wake isipokuwa kwa mambo mawili hivi ambayo Mungu alimsamehe.

Thibitisho: "Lakini sasa ufalme wako hautadumu; BWANA amejitafutia mtu aupendezaye moyo wake, naye BWANA amemwamuru yeye kuwa mkuu juu ya watu wake, kwa sababu wewe hukulishika neno lile BWANA alilokuamuru" (1 Samweli 13:14). "Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote" (Matendo 13:22). "…kwa sababu Daudi alifanya yaliyo mema machoni pa BWANA, wala hakukosa katika yote aliyomwamuru, siku zote za maisha yake, isipokuwa katika habari ya Uria, Mhiti" (1 Wafalme 15:5).

120. Ni wafalme wangapi waliokikalia kiti chake cha enzi baada yake? Taja majina yao.

Jibu: Kulikuwepo na wafalme ishirini (20) baadaye, wote wakiwa ni wa uzao huo huo wa Daudi. Majina yao: Solomon, Rehoboamu, Abija, Asa, Yehoshofati, Yoram, Azia, Yoashi, Amazia, Uzaya, Yothamu, Ehaz, Hezekia, Manase, Amon, Yosia, Yohohazi, Yehoakim, Yehoakin na Zedekia.

Thibitisho: Vitabu vya Wafalme na Mambo Ya Nyakati.

KUHUSU KUGAWANYIKA KWA UFALME

SEHEMU MBILI

121. Je, wafalme hawa wote tuliowataja walitawala makabila kumi na mbili ya Israeli kama alivyofanya Daudi?

Jibu: Sulemani alitawala kweli lakini baada ya kifo chake, na kama adhabu kwa kosa lake, makabila kumi yakauasi ufalme chini ya wana wa Daudi na wakausimamisha ufalme wao wenyewe-Yereboam mwana wa Nebat aliyeusimamisha ufalme mwingine sehemu ya kaskazini mwa Israeli ukiwa na makabila kumi.

Thibitisho: "Basi mfalme Sulemani akawa mfalme juu ya Israeli wote" (1 Wafalme 4:1). "Kwa hiyo BWANA akamwambia Sulemani, Kwa kuwa umefanya hayo, wala hukuyashika maagano yangu, na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme usiwe wako, nami nitampa mtumishi wako. Walakini katika siku zako sitafanya haya, kwa ajili ya Daudi baba yako; nitaurarua utoke katika mkono wa mwana wako. Lakini sitauondoa ufalme wote pia; nitampa mwana wako kabila moja, kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, na kwa ajili ya Yerusalemu niliouchagua" (1 Wafalme 11:11-13). 1 Wafalme 12:1-9.

122. Ufalme huo ulikuwa na makabila kumi yapi?

Jibu: Efraimu, Manase, Isakari, Zabuloni, Naftali, Ashur, Dani, Gadi, Simioni na Rubeni.

Thibitisho: 1 Ufalme 11:29-35 na mahali pengine pengi.

123. Ufalme mpya uliitwaje?

Jibu: Ufalme wa Israeli. Pia ilikuwa ikitajwa na manabii wa Israeli kama Efraimu kutokana na kabila liliongoza kujitenga.

Thibitisho: Kitabu cha Wafalme na cha Hosea.

124. Je, huu ufalme mpya ulitawaliwa kwa sheria zile zile za Musa kama siku za Daudi?

Jibu: La. Yeroboamu alifutilia mbali sheria za Musa na akawaongoza makabila hayo kumi kuabudu miungu, jambo ambalo hawakuliacha.

Thibitisho: "Yeroboamu akasema moyoni mwake, Basi ufalme utairudia nyumba ya Daudi. Kama watu kawa wakipanda kwenda kutoa dhabihu katika nyumba ya BWANA huko Yerusalemu, ndipo mioyo ya watu hawa itamrudia bwana wao, yaani Rehoboamu, mfalme wa Yuda; nao wataniua mimi, na kumrudia Rehoboamu, mfalme wa Yuda. Kwa hiyo mfalme akafanya shauri, akafanyiza ng'ombe wawili wa dhahabu, akawaambia watu, Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo miungu yenu, enyi Israeli, iliyowapandisha kutoka nchi ya Mirsri. Akamweka mmoja katika Betheli, na wa pili akamweka katika Dani. Jambo hili likawa dhambi, maana watu walikwenda kuabudu mbele ya kila mmoja, hata huko Dani" (1 Wafalme 12:26-30).

125. Walfame wangapi walitawala ufalme wa kaskazini wa makabila kumi? Taja majina yao.

Jibu: Wafalme waliotawala baada ya Yeroboam walikuwa 18 kwa ujumla. Nedab, Baasha, Ila, Zimri, Omura, Ahab, Ahazia, Yoram, Yehu, Yehuazi, Yoash, Yeroboam, Zekeria, Shalom, Menahem, Pikahaya, Pika na Hoshea.

Thibitisho: Kitabu cha Wafalme.

126. Ni makabila gani yaliyokuwa upande wa ufalme baada ya kujitenga kwa wengine?

Jibu: Benjamin na Yuda.

Thibitisho: "Na ndani ya miji yote mmoja mmoja aliweka ngao na mikuki, akaifanya kuwa na nguvu nyingi mno. Yuda na Benyamini ikawa milki yake" (2 Mambo Ya Nyakati 11:12).

127. Wale waliokuja kutawala ufalme kufuata mkondo wa Daudi walijulikana kwa jina gani, na ufalme huo ulichukua muda gani?

Jibu: Ufalme wa Daudi ulijulikana kama ufalme wa Yuda. Ilichukua muda wa miaka 393 baada ya kujitenga kwa makabila yale kumi. Ufalme huu uliharibiwa na mfalme wa Babeli, Nebukadneza aliyewatwa watu na kuwapeleka Babeli, ambako walikaa kama mateka kwa miaka 70. Baadaye wana wa Yuda wakarejeshwa kwao chini ya uongozi wa Ezra na Nehemia, mfalme wa Uajemi (Cyrus) alipotangaza kurudishwa kwao, ambaye alikuwa ameupindua utawala wa Babeli. Lakini ufalme wa Daudi haukurudia hali yake ya kitambo. Miaka 540 baada ya marejeo yao wana wa Israeli kutoka Babeli,Yesu akazaliwa. Miaka 70 baadaye, Warumi waliliangamiza jimbo la Waisraeli, na tangu hapo Watu wa mataifa wameukanyagia chini.

Thibitisho: Vitabu vya Mambo ya Nyakati, Ezra, Nehemia, Mathayo na Luka.

KUHUSU AGANO KWA DAUDI

128. Je, Mungu alizungumzia juu ya ufalme masikioni mwa Daudi?

Jibu: Ndio. Aliahidi kumpa mwana ambaye angekikalia kiti chake cha enzi milele, na aimarishe ufalme katika Israel ambao haungekuwa na mwisho; na Daudi angeyaona haya na pia kuwa katika ufalme huo.

Thibitisho: "Je! sivyo ilivyo nyumba yangu mbele za BWANA? Kwa kuwa amefanya nami agano la milele; ina taratibu katika yote, ni thabiti, maana ni wokovu wangu wote, na shauku langu lote" (2 Samweli 23:5). "BWANA amemwapia Daudi neno la kweli, hatarudi nyuma akalihalifu, baadhi ya wazao wa mwili wako nitawaweka katika kiti chako cha enzi" (Zaburi 132:11). "Nimefanya agano na mteule wangu, nimemwapia Daudi, mtumishi wangu. Wazao wako nitawafanya imara milele, nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele" (Zaburi 89:3-4). "Mimi sitalihalifu agano langu, sitalibadili neno liliotoka midomoni mwangu" (Zaburi 89:34). "Kitathibitika milele kama mwezi; shahidi aliye mbinguni mwaminifu,…" (Zaburi 89:37). "Na nyumba yako, na ufalme wako, vitathibitishwa milele mbele yako. Nacho kiti chako kitafanywa imara milele (2 Samweli 7:16).

129. Je, agano hili na Daudi limetimizwa?

Jibu: Ilitimizwa kiasi katika Sulemani; lakini utimilifu haswa utakuwa katika Kristo, aliyezaliwa katika ukoo ule wa Daudi ambaye ni mwana wa Mungu na pia mwanadamu, Daudi, mrithiwake.

Thibitisho: "Basi BWANA amelitimiza neno lile alilolinena; nami nimesimama mahali pa Daudi baba yangu, na kuketi katika kiti cha enzi cha Israeli, kama BWANA alivyoahidi, nami nimeijenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli" (1 Wafalme 8:20). "Waume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo. Basi kwa kuwa ni nabii, akijua ya kuwa Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa viuno vyake atamketisha mmoja katika kiti chake cha enzi;…" (Matendo 2:29-30). "Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu" (Mathayo 1:1). "Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake" (Luka 1:32).

130. Kristo basi atakikalia kiti cha enzi cha Daudi?

Jibu: Atakikalia. Atakapokuja mara ya pili atakikalia kiti cha enzi na atawale kutoka Yerusalemu kama mfalme wa Wayahudi na wa watu wote pia.

Thibitisho: "Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;…"(Mathayo 25:31). "Maongeo ya enzi yake na amani hayatakuwa na mwisho kamwe, katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; kuuthibitisha na kuutegemeza kwa hukumu na kwa haki, tangu sasa na hata milele. Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo" (Isaya 9:7). "Katika siku zile, na wakati ule, nitamchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atafanya hukumu na haki katika nchi hii. Katika siku zile Yuda ataokolewa, na Yerusalemu utakaa salama; na jina lake atakaloitwa ni hili, BWANA ni haki yetu: (Yeremia 33:15, 16). "Ndipo mwezi utatahayari, na jua litaona haya; kwa kuwa na mbele ya wazee wake kwa utukufu" (Isaya 24:23). "Wakati ule watauita Yerusalemu kiti cha enzi cha BWANA; na mataifa yote watakusanyika huko Yerusalemu, kwa ajili ya jina la BWANA; wala hawatakwenda tena kwa ukaidi wa moyo wao mbaya" (Yeremia 3:17). "Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa BWANA, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA katika Yerusalemu" (Isaya 2:3). "Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, watumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo haitapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa" (Danieli 7:14).

131. Kristo yuarudi tena duniani mara ya pili?

Jibu: Ndio. Atarudi jinsi hiyo alivyokwenda au kupaa. Na atakapokuja watu watamuona waziwazi.

Thibitisho: "…wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni" (Matendo 1:11). "…ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu" (Matendo 3:21). "…na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake; katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu; watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake; yeye atakapokuja ili kutukuzwa katika watakatifu wake, na kustaajabiwa katika wote waliosadiki katika siku ile, (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu)" (2 Wathesalonike 1:7-10). "Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo" (1 Yohana 3:2). "Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina" (Ufunuo 1:7).

KUHUSU UFUFUO, JUKUMU (WAJIBU) NA HUKUMU

132. Kristo atafanya nini mara atakaporudi tena?

Jibu: Atawakusanya wote wanaostahili hukumu wawe hai au waliolala mauti. Wafu atawafufua kutoka kwa makaburi yao; walio hai atawakusanya kupitia kwa malaika. Wote imewapasa kusimama mbele ya kiti chake cha enzi, ili wapate kupokea kwa miili yao hukumu wanayostahili.

Thibitisho: "Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake;…" (2 Timotheo 4:1). "Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele" (Danieli 12:2). "Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu" (Yohana 5: 29). "Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,…" (1 Wakorintho 15:51). "Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo" (1 Wathesalonike 4:17). "Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya" (2 Wakorintho 5:10). "Lakini wewe Je! mbona wamhukumu ndugu yako? au wewe je! mbona wamdharau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu" (Warumi 14:10). "Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu" (Warumi 14:12).

133. Ni nani wanastahili hukumu?

Jibu: Wote wanaoufahamu Ukweli wawe wameukubali au wameukataa.

Thibitisho: "Aaminiye an kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa" (Marko 16:16). "Kwa maana sisi tu manukato ya Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea; katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Naye ni nani atoshaye kwa mambo hayo (2 Wakorintho 2:15-16). "Nasi twajua ya kuwa hukumu ya Mungu ni ya kweli juu yao wafanyao hayo" (Warumi 2:2). "…na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma watapata hasira na ghadhabu; dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Myunani pia;…" (Warumi 2:8-9). "…katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu" (Warumi 2:16). "Na hili ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu" (Yohana 3 19). "Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho" (Yohana 12:48).

134. Je, kuna wengine wasiotahili kusimama mbele ya kiti cha hukumu?

Jibu: Ndio, wengi. Ni nuru inayomfanya mtu awe anastahili; lakini giza kimetanda dunia; na palipo na giza hapana dhambi ya kukemewa.

Thibitisho: "Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakin sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa" (Yohana 9:41). "Mwanadamu mwenye heshima, iwapo hana akili, amefanana na wanyama wapoteao" (Zaburi 49:20). "Kwa sababu sheria ndiyo ifanyayo hasira; maana pasipokuwapo sheria, hapana kosa" (Warumi 4:15). "…maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria;…" (Warumi 5:13). "Kama nisingalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi yao" (Yohana 15:22). "Maana, tazama, giza litaifunika dunia, na giza kuu litazifunika kabila za watu; bali BWANA atakuzukia wewe, na utukufu wake utaonekana juu yako" (Isaya 60:2).

135. Wale wasiostahili kusimama hukumuni ni yapi yatakayowapata?

Jibu: Hufa na kusahauliwa kama kwamba hawakuwepo asilani.

Thibitisho: "Atakwenda kwenye kizazi cha baba zake; hawataona nuru hata milele" (Zaburi 49:19). "Nami nitawalevya wakuu wake, na watu wake wenye hekima, maliwali wake, na maakida wake, na mashujaa wake; nao watalala usingizi wa milee, wasiamke, asema Mfalme, BWANA wa majeshi, ambaye jina lake ni BWANA" (Yeremia 51:57). "Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajilia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao" (Isaya 26:14). "Miongoni mwao waliokufa nimetupwa, kama waliouawa walalao makaburini. Hao ambao Wewe huwakumbuki tena, wametengwa mbali na mkono wako" (Zaburi 88:5). "Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;…" (Warumi 5:12). "…ambao akili zao zimetiwa giza, nao wamefarikishwa na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao:…" (Waefeso 4:18).

136. Wale wenye haki kati ya wale wanausimama hukumuni watapewa nini?

Jibu: Miili isiyokufa, miili ya ya kufa itageuzwa kufumba na kufumbua jicho.

Thibitisho: "…atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake" (Wafilipi 3:21). "Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa" (1 Wakorintho 15:53). "Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni; ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi. Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima" (2 Wakorintho 5: 2-4). "Lakini, ikiwa Roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu…" (Warumi 8:11). "…wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, watapewa uzima wa milele;…" (Warumi 2:7). "Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele" (Wagalatia 6:8).

137. Watakaokataliwa mbali ni yapi yatakayowafika?

Jibu: Wataondoka mbele yake wakiwa wameaibika na fedheha tele, na kuteseka kama vile hakimu atavyoona wastahili na hatimaye waangamizwe kwa mauti ya pili.

Thibitisho: "Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;…" (Mathayo 25:41). "Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje" (Luka 13:28). "Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele" (Danieli 12:2). "Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana. Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi" (Luka 12:47-48). "Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto" (Ufunuo 20:15). "Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili" (Ufunuo 21:8). "Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele" (Wagalatia 6:8). "Ni faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti" (Warumi 6:21).

KUHUSU KRISTO MWANGAMIZI WA MATAIFA

NA KUWAREJESHEA WAISRAELI HALI

YAO YA AWALI

138. Kristo akishawakatia kesi wale wanaosimama mbele yake, atafanya kitu gani kingine?

Jibu: Atashambulia mataifa ya ulimwengu ili kuwafanya wamtii.

Thibitisho: "Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake" (Ufunuo 19:19). "Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana-Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme; na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu" (Ufunuo 17:14). "Nalikanyaga shinikizoni peke yangu; wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami; naam, naliwakanyaga kwa hasira yangu, naliwaponda kwa ghadhabu yangu; na mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu yao, nami nimezichafua nguo zangu zote. Maana siku ya kisasi ilikuwamo moyoni mwangu, na mwaka wao niliowakomboa umewadia" (Isaya 63:3-4). "Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita" (Ufunuo 19:11). "Utawaponda kwa fimbo ya chuma, na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi" (Zaburi 2:9).

139. Mataifa yakisha kupinduliwa ni kipi kingine atakachokifanya?

Jibu: Atawakusanya tena Wayahudi toka nchi walikotawinyika, na wapewe nchi yao wenyewe tena.

Thibitisho: "Nami nitauweka utukufu wangu kati ya mataifa, na mataifa wote wataiona hukumu yangu niliyoitekeleza, na mkono wangu niliouweka juu yao. Basi, nyumba ya Israeli watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA Mungu wao, tangu siku hiyo na baadaye. Nao mataifa watajua ya kuwa nyumba ya Israeli walihamishwa, na kwenda kifungoni, kwa sababu ya uovu wao; kwa sababu waliniasi, nami nikawaficha uso wangu; basi nikawatia katika mikono ya adui zao, nao wakaanguka kwa upanga, wote pia. Kwa kadiri ya uchafu wao, kwa kadiri ya makosa yao, ndivyo nilivyowatenda, nami nikawaficha uso wangu. Kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Sasa nitawarejeza watu wa Yakobo waliohamishwa, nitawahurumia nyumba yote ya Israeli; nami nitalionea wivu jina langu takatifu" (Ezekieli 39:21-25). "Lisikieni neno la BWANA, enyi mataifa, litangazeni visiwani mbali; mkaseme, Aliyemtawanya Israeli atamkusanya, na kumlinda, kama mchungaji alindavyo kundi lake" (Yeremia 31:10). "Naye atawatwekea mataifa bendera, atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za dunia" (Isaya 11:12). "Ukawaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitawatwaa wana wa Israeli toka kati ya mataifa walikokwenda, nami nitawakusanya pande zote, na kuwaleta katika nchi yao wenyewe; nami nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi hiyo, juu ya milima ya Israeli; na mfalme mmoja atakuwa mfalme wao wote; wala hawatakuwa tena mataifa, mawili, wala hawatagawanyikana kuwa falme mbili tena, hata milele" (Ezekieli 37:21-22).

140. Wayahudi wote watarejeshwa?

Jibu: Wote watakusanywa toka nchi za mataifa lakini sio wote watakaoingia nchi yao wenyewe. Wale wasiotii watang'olewa kati ya wengine kama ilivyokuwa kuja kwao toka Misri chini ya Musa.

Thibitisho: "…nami nitawatoa katika mataifa, na kuwakusanya, na kuwatoa katika nchi mlizotawanyika ndani yake, kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa ghadhabu iliyomwagika;…" (Ezekieli 20:34). "Nami nitawasafisha kwa kuwatoa waasi, na hao walionikosa; nitawatoa katika nchi wanayokaa ugenini, lakini hawataingia katika nchi ya Israeli; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA" (Ezekieli 20:38). "Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema BWANA wa majeshi" (Malaki 3:5). "…nami nitakuelekezea wewe mkono wangu, na kukutakasa takataka zako kabisa, na kukuondolea bati lako lote; nami nitarejeza upya waamuzi wako kama walivyokuwa hapo kwanza, na washauri wako kama hapo mwanzo; baada ya hayo utaitwa, Mji wa haki, mji mwaminifu" (Isaya 1:25-26).

141. Wayahudi watakuwa ni taifa takatifu, lenye haki wakati wa kuimarishwa kwao?

Jibu: Ndio. Agano jipya litafanyika na kwa njia hii dhambi zao zitasamehewa kabisa na sheria ya Mungu itaandikwa ndani ya nyoyo zao. Wote watamjua na kumpenda Mungu mdogo kwa mkubwa.

Thibitisho: "Watu wako nao watakuwa wenye haki wote, nao watairithi nchi milele; chipukizi nililolipanda mimi mwenyewe, kazi ya mikono yangu mwenyewe, ili mimi nitukuzwe" (Isaya 60:21). "Angalia, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema BWANA. Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema BWANA; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue BWANA; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema BWANA; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena" (Yeremia 31:31-34).

142. Kutakuwepo na hekalu mpya katika siku hizo za furaha?

Jibu: Ndio. Hekalu la ajabu ambalo halijawahi kuonekana duniani. Nchi itakuwa kama paradiso na hekalu itakuwa katikati ya nchi mahali ambapo Mungu amejitengea kama patakatifu pake. Watu watakuwa wakizuru kila mara mahali hapa ili wajifunze kumtumikia Bwana.

Thibitisho: Ezekieli 40-48. "Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema BWANA wa majeshi; na katika mahali hapa nitawapa amani, asema BWANA wa majeshi" (Hagai 2:9). "Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, kondoo waume wa Nebayothi watakutumikia; watapanda juu ya madhabahu yangu kwa kibali, nami nitaitukuza nyumba ya utukufu wangu" (Isaya 60:7). "Utukufu wa Lebanoni utakujia wewe, mberoshi na mtidhari na mteashuri pamoja; ili kupapamba mahali pangu patakatifu, nami nitapatukuza mahali pa miguu yangu" (Isaya 60:13). "Tena itakuwa siku hiyo, ya kwamba nuru yake haitakuwa na mwangaza na kiwi;…" (Zekaria 14:6). "Hii ndiyo adhabu ya Misri, na adhabu ya mataifa yote, wasiokwea ili kushika sikukuu ya Vibanda" (Zekaria 14:19). "Nao watasema, Nchi hii, iliyokuwa ukiwa, imekuwa kama bustani ya Adeni; nayo miji iliyokuwa mahame, na ukiwa, na magofu, sasa ina maboma, inakaliwa na watu" (Ezekieli 36:35). "Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi" (Mika 4:1). "Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, naye atawakemea mataifa wenye nguvu walio mbali; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitanua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe" (Mika 4:3).

KUHUSU MATAIFA MENGINE KIPINDI CHA UTAWALA WA KRISTO

143. Ni uhusiano gani utakaokuwepo kati ya mataifa mengine na lile la Wayahudi wakati wa Ufalme huu mpya?

Jibu: Mataifa yote ya ulimwengu yatatiishwa chini ya mamlaka ya Kristo na wawape heshima Wayahudi kwa baraka ambazo watazishiriki kwa ajili yao.

Thibitisho: "Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo haitapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa" (Danieli 7:14). "Kwa maana kila taifa na ufalme wa watu wasiotaka kukutumikia wataangamia; naam, mataifa hayo wataharibiwa kabisa" (Isaya 60:12). "Wakati huo nitawaingizeni, na wakati huo nitawakusanya; kwa maana nitawafanya ninyi kuwa sifa na jina, miongoni mwa watu wote wa dunia, nitakapowarudisha wafungwa wenu mbele ya macho yenu, asema BWANA" (Sefania 3:20). "BWANA wa majeshi asema hivi, Siku hizo watu kumi, wa lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi; naam, wataushika wakisema, Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi" (Zekaria 8:23).

144. Utawala huu wa Kristo na watu wake juu ya mataifa yote utachukua muda gani?

Jibu: Miaka 1000.

Thibitisho: "Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu" (Ufunuo 20:4). "Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu" (Ufunuo 20:6).

145. Watu wa mataifa watakuwa na miili inayokufa au miili ya milele isiyokufa?

Jibu: Hakuna atakayekuwa na mwili usiokufa isipokuwa Kristo na watakatifu wake. Watu watakuwa wakifa kama wakati huu, ila uhai utakuwa mrefu kuliko sasa na maisha yatakuwa matamu zaidi.

Thibitisho: "Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa" (Isaya 65:20). "Wala hawataoa wanawake wajane, wala mwanamke aliyeachwa na mume wake; lakini watatwaa mabikira wa wazao wa nyumba ya Israeli, au mjane aliyefiwa na mumewe kuhani" (Ezekieli 44:22). "Wala hawatakaribia maiti na kujitia unajisi; ila kwa ajili ya baba, au mama, au mwana, au binti, au ndugu mwanamume, au ndugu mwanamke asiyeolewa bado, waweza kujitia unajisi" (Ezekieli 44:25).

KUHUSU MWISHO WA MIAKA ELFU-MOJA

146. Ufalme utafikia kikomo au hatima yake mwisho wa miaka 1000?

Jibu: Ufalme hautaisha; lakini mambo yatabadilika mwisho wa miaka hiyo elfu.

Thibitisho: "Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote" (1 Wakorintho 15:28).

147. Ni mambo gani yatakayobadilika wakati huo?

Jibu: Mambo yote yatakayobadilika hatuyajui; ila twajua kuwa mauti itaangamizwa duniani na kuwa Kristo atarejesha mamlaka ya ufalme kwa baba, ili Mungu awe yote katika wote.

Thibitisho: "Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti" (1 Wakorintho 15:26). "Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo,wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita" (Ufunuo 21:4). "Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake" (1 Wakorintho 15:24-25).

148. Kuangamizwa kwa mauti kutatokeaje mwisho wa miaka hiyo elfu?

Jibu: Watu wote wakishapata miili isiyoweza kufa, watu ambao kuambatana na Mungu katika miaka hiyo elfu. Lakini wale ambao hawaambatani na Mungu, wataangamizwa.

Thibitisho: "Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli. Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure. Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili" (Ufunuo 21:5-8). "BWANA huwahifadhi wote wampendao, na wote wasio haki atawaangamiza" (Zaburi 145:20). "Wabaya wa nchi pia umewaondoa kama takataka, ndiyo maana nimezipenda shuhuda zako" (Zaburi 119:119). "Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto" (Ufunuo 20:14).

149. Je, itawezekana wale ambao wana miili ya kufa katika ufalme wa Kristo, kupata miili ya milele isiyokufa mwisho wa miaka elfu moja?

Jibu: Ndio. Ikiwa watampendeza Mungu, watapata uzima wa milele mwisho wa miaka hiyo elfu kama vile walewanaoupata uzima huo mwanzo wa miaka hiyo. Wakifa kabla ya wakati huo, basi watafufuliwa na kupokea utukufu huo. Kama wangali wazima watageuzwa. Hesabu au idadi yao itazidi idadi yao wale waliopokea uzima wa milele mwanzoni. Watakuwa ni mavuno, hali wale waliokubaliwa mwanzo watakuwa limbuko lao.

Thibitisho: "Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti" (1 Wakorintho 15:26). "…katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa" (Ufunuo 22:2). "Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao" (Ufunuo 20:12). "Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo" (Ufunuo 14:4).

150. Mauti ikishaangamizwa hivi kutoka duniani, dunia itaharibiwa?

Jibu: La. Dunia yadumu milele, na itajawa na utukufu wa Bwana na furaha ya watu wake.

Thibitisho: "Wala hapatakuwa na laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake watamtumikia; nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao. Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele" (Ufunuo 22:3-5). "Kwa maana dunia itajazwa maarifa ya utukufu wa BWANA, kama maji yaifunikavyo bahari" (Habakuki 2:14). "Akajenga patakatifu pake kama vilele, kama dunia aliyoiweka imara milele" (Zaburi 78:69). "Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, na miisho ya dunia kuwa milki yako " (Zaburi 2:8). Zaburi 37:11-18. "Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele" (Ufunuo 11:15).

MAJIBIZANO KWA WATOTO

1. Ni nani aliyeumba vitu vyote?

Jibu: Mungu.

2. Mungu yuko wapi?

Jibu: Yuko Mbinguni.

3. Je, Yuko kwingine kote?

Jibu: Ndio. Yu kila mahali.

4. Mungu anawezeji kuwa kila mahali ikiwa yu mbinguni?

Jibu: Kwa roho wake; huujaza ulimwengu hivi.

5. Roho wa Mungu ni nini?

Jibu: Ni nguvu zisizoonekana kwayo ulimwengu na vitu vyote viliumbwa.

6. Mungu mwenyewe ni nani?

Jibu: Ni kiumbe kitukufu.

7. Anaitwaje?

Jibu: Baba.

8. Kwa nini anaitwa Baba?

Jibu: Kwa sababu vitu vyote vinatokana naye na ni vyake. Aliviumba vyote.

9. Je, Mungu ni mbali na Roho wake?

Jibu: La, ni wamoja kama vile moto na miali yake ilivyo, au jua na mwangaza wake.

10. Mungu anaweza kutuona akiwa mbinguni?

Jibu: Ndio. Anaweza kutuona na kusikia yote tuyanenayo. Roho wake yu kila mahali na vitu vyote vi ndani yake. Kwa hivyo anafahamu yote yanayotendeka. Hakuna kitu kinachoweza kusitirika mbele yake.

11. Je, anayajua hata mawazo yetu?

Jibu: Ndio, anayajua mawazo yetu hata kama hatuyataji.

12. Haya yanatufunza nini?

Jibu: Tufanye hadhara tunapozungumza, kufikiri au kutenda lo lote lile.

13. Je, Mungu anatuhitaji kuwa na mwenendo fulani maishani?

Jibu: Ndio. Anataka tumtii.

14. Ametwambia tunayopaswa kutenda?

Jibu: Ndio.

15. Wapi?

Jibu: Katika Biblia.

16. Biblia ni nini?

Jibu: Ni kitabu ambacho kimeandikwa na watu kadhaa walioongozwa kwa pumzi ya Mungu kuandika yanayopasa.

17. Tunajifunza nini kutoka kwa Biblia?

Jibu: Tunajifunza mambo ambayo Mungu amefanya na kusema siku zilizopita, anayotazamia kufanya wakati huu; na atakayoyafanya siku za usoni.

18. Mungu amefanya mambo gani siku zilizopita?

Jibu: Alimuumba mtu na kumweka duniani.

19. Ni muda gani umepita tangu haya kutendeka?

Jibu: Kama miaka 6,000 iliyopita.

20. Taja majina ya mtu na mkewe walioumbwa mwanzo.

Jibu: Adamu na Eva.

21. Mungu aliwaweka wapi alipowaumba?

Jibu: Katika bustani maridadi ya Eden iliyojaa miti mingi ya matunda.

22. Aliwapa maagizo yapi?

Jibu: Aliwaagiza kula matunda ya miti iwayo yote ila ya mti mmoja katikati ya bustani, wasiuguze.

23. Walitii?

Jibu: Hawakutii kwani waliyala matunda ya mti uliokuwa katikati ya bustani.

24. Matokeo ya kutotii kwao yalikuwaje?

Jibu: Walihukumiwa kifo, na wakafukuzwa kutoka bustanini wakajitafutie chakula kwa jasho.

25. Tunashiriki hukumu hii?

Jibu: Ndio, kwa kuwa sisi ni wana wao. Tumetokana nao. Hukumu hiyo ilikuwa laana juu ya miili yao. Miili ambayo sisi nasi tunayo.

26. Mungu alimwambia nini Adamu?

Jibu: "U mavumbi na mavumbini utarudi."

27. Mungu alimuumba Adamu kutoka mavumbini?

Jibu: Ndio. "Mungu alimuumba mtu kutoka kwa mavumbi ya ardhi, na akampulizia puani mwake pumzi yenye uhai, na mtu akawa nafsi hai."

28. Ni kweli kama wasemavyo watu kuwa Mungu alimpulizia Adamu roho isiyoweza kufa?

Jibu: La. Sivyo kabisa, kwani mwanadamu ni kiumbe cha kufa kwa sababu ya dhambi.

29. Dhambi ni nini?

Jibu: Kutotii amri ya Mungu.

30. Mwanadamu hufa?

Jibu: Ndio, mtu hufa na kuurudia udongo, na pumzi humrudia Mungu aliyeitoa.

31. Pumzi inayomrudia Mungu ni nini?

Jibu: Ni uzima wa Mungu ambao hutupulizia ili tuwe hai. Sio sisi ila ni kitu kinachotupa uhai.

32. Mungu anapouchukua uhai huu mtu anaweza kuendelea kuishi au hata kuwa na kumbukumbu?

Jibu: La hasha, mwanadamu hufa, hana kumbukumbu tena, mpaka wakati wa kurudishiwa uhai huo wakati wa ufufuo.

33. Je, ni kweli kuwa tunapokufa sisi huenda mbinguni au jehanam (motoni) kama wafundishavyo madhehebu fulani?

Jibu: La. Haya ni mafunzo namna ya hekaya au hadithi tu zinazofunzwa na madhehebu. Tunapokufa huenda makaburini na kungojea ufufuo.

34. Ufufuo ni nini?

Jibu: Ni kupata uhai tena kwa watu waliofufuliwa toka kwa wafu.

35. Ufufuo utakuwepo?

Jibu: Ndio, Mungu ameahidi kuwafufua watu wake toka kwa wafu.

36. Watu wake ni akina nani?

Jibu: Wote wanaomjua na kumwamini, wote wanaomtii na kushika amri zake.

37. Ni watu wake tu watakaofufuliwa kutoka kwa wafu?

Jibu: Wema na waovu watafufuliwa.

38. Watu wote waliowahi kuishi na kufa watafufuliwa?

Jibu: La, ni wale tu wanaostahili watakaofufuliwa.

39. Ni akina nani hao wanaostahili?

Jibu: Ni wale wanaujua ukweli na mapenzi ya Mungu wawe ni watiifu au wawe ni wasiotii.

40. Yatakayowapata wale wasiostahili ni yapi?

Jibu: Hawataonekana wala kusikika tena. Wanapokufa wanapotea kana kwamba hawakuishi kabisa.

41. Mungu atawapa nini wale watakaompendeza Mungu wakati wa ufufuo.

Jibu: Watageuzwa. Miili yao yakuharibika itageuzwa isiharibike. Hawateendelea kuwa na miili ya kufa bali watavishwa miili ya milele isiyokufa. Hawataweza kupatwa na mauti tena.

42. Wale wasiompendeza Mungu wakati huo watafanywaje?

Jibu: Watafukuzwa waende zao kwa aibu na dhihaka, wateseke, kwa muda mfupi au mrefu kama atakavyochagua Mungu; halafu wafe tena.

43. Ni nani atakayefanya kazi hii kubwa ya kufufua wafu na kuwahukumu?

Jibu: Ni Mungu.

44. Ni Mungu mwenyewe atakayeifanya kazi hiyo ama itashughulikiwa na mwingine?

Jibu: Kupitia kwa mwingine.

45. Kupitia kwa nani?

Jibu: Yesu Kristo.

46. Yesu Kristo ni nani?

Jibu: Ni mwana wa Mungu.

47. Alizaliwa lini?

Jibu: Zamani sana.

48. Muda gani tangu azaliwe?

Jibu: Zaidi ya miaka 1900 sasa.

49. Alizaliwa wapi?

Jibu: Bethlehemu.

50. Bethlehemu i wapi?

Jibu: Katika nchi takatifu.

51. Nchi takatifu iko wapi?

Jibu: Ni upande wa mashariki wa Bahari kuu, nchi ya Palestina.

52. Kwa nini yaitwa nchi takatifu?

Jibu: Kwa sababu Mungu aliichagua na kuwapa wazee (baba) wakuu.

53. Hawa akina baba ni nani?

Jibu: Ibrahimu, Isaka na Yakobo.

54. Waliishi kitambo gani?

Jibu: Karibu miaka 3700 iliyopita.

55. Waliishi katika nchi hiyo takatifu?

Jibu: Ndio, lakini Ibrahimu hakuwa kule mwanzoni. Alikuwa akishi katika nchi ya Wakaldayo upande wa mashariki.

56. Ni kitu gani kilichomfanya aende katika nchi takatifu.

Jibu: Kwa sababu Mungu alimwambia afanye hivyo.

57. Ni ahadi gani aliyompa Ibrahimu alipofika nchi hiyo takatifu?

Jibu: Mungu angemfanya kuwa taifa kuu.

58. Alimuahidi kitu kingine cho chote?

Jibu: Mungu angembariki na mataifa yote kupitia kwake.

59. Ahadi nyingine ye yote?

Jibu: Mungu angempa nchi takatiku iwe urithi wake milele.

60. Ahadi hizo zimetimizwa?

Jibu: Sehemu fulani tu.

61. Sehemu gani hiyo?

Jibu: Ibrahimu alikuja kuwa taifa kubwa kweli, na sehemu fulani ya baraka imewafikia mataifa kwa njia ya mwana au uzao wa Ibrahimu, Yesu. Lakini bado Ibrahimu atakuwa taifa kuu zaidi, na baraka zisizoelezeka zitawajia watu wote wa mataifa siku zijazo.

62. Ibrahimu amepokea na kurithi nchi takatifu milele kama alivyoahidiwa?

Jibu: La. Ibrahimu alikufa; na alipokuwa hai, alikuwa mgeni tu katika nchi hiyo ya ahadi.

63. Mungu atatimiza ahadi yake juu ya jambo hili?

Jibu: Ndio. Ahadi ya Mungu haiwezi kupita bure. Ibrahimu, Isaka na Yakobo watafufuka toka kwa wafu na kupokea urithi wa nchi hiyo, Kristo atakapokuwa mtawala wa nguvu na utukufu wa ajabu.

64. Isaka alikuwa nani?

Jibu: Mwana wa Ibrahimu.

65. Yakobo alikuwa nani?

Jibu: Mwana wa Isaka.

66. Yakobo alikuwa na wana wangapi?

Jibu: Kumi na mbili.

67. Taja majina yao?

Jibu: Rubeni, Simioni, Levi, Yuda, Isakari, Zebulon, Yusufu, Benyamini, Dani, Naftali, Gadi, na Asheri.

68. Mambo gani yaliwapata hawa?

Jibu: Walienda kwa kushuka Misri na huko wakazaana na kuongezeka sana na kuwa taifa kubwa.

69. Wamisri waliwatendea mema?

Jibu: La. Farao mfalme wa Misri aliwatenda mabaya.

70. Walikaa Misri muda wa miaka mingapi?

Jibu: Kati ya miaka 200 na 300.

71. Mungu aliwaokoa?

Jibu: Ndio.

72. Kwa njia gani?

Jibu: Alimtuma Musa kuwaadhibu Wamisri kwa mapigo na kuwatoa Waisraeli kutoka huko.

73. Kwa nini waliitwa Waisraeli?

Jibu: Kwa sababu jina hili Israeli lilikuwa la baba yao Yakobo alilopewa na Mungu; maana ya jina lenyewe-Mwana wa kifalme wa Mungu.

74. Ni mapigo mangapi yaliyowapata Wamisri?

Jibu: Kumi, mapigo makubwa na ya kutisha.

75. Ni kitu gani kilichotendeka Musa alipowatoa wana wa Israeli kutoka huko?

Jibu: Wamisri waliwafukuza katika kuwafuatia, na walikuwa karibu kuwashika na kuwarejesha.

76. Mungu alifanya kitu gani hata kikawazuia Wamisri wasiwashike Waisraeli.

Jibu: Aliwaachilia Waisraeli wapite katika nchi kavu bahari ilipojitenga, na wakisha vuka salama, Wamisri waliwafuatia katika njia ile kavu, na hapo ndipo bahari iliporejea na wote wakazama maji.

77. Kwa nini Mungu alifanyiza miujiza hii yote?

Jibu: Kuonyesha nguvu zake kwa Waisraeli na mataifa yote, ili Waisraeli na dunia nzima ijue kuwa yu Mungu, Muumba mbingu na nchi.

78. Jeshi nzima la Misri lilipozama maji na jambo gani lililotukia?

Jibu: Musa aliwaongoza waisrael nyikani kwenye mabonde na milima, mlima wa Sinai, na hapo Mungu akajidhihirisha kwao kwa moto na wingu. Moshi na tufani na akawapa sheria nzuri wazishike.

79. Watu wengi hawa walipataje chakula jangwani?

Jibu: Mungu aliwanyeshea mana kila usiku, na watu waliamka kila asubuhi kwenda kuikiota mana hiyo na kuiweka vikapuni.

80. Walikuwa nyikani muda gani?

Jibu: Miaka arobaini.

81. Walienda wapi baadaye?

Jibu: Waliiendea nchi ya ahadi. Yoshua alikuwa kiongozi wao baada ya kifo cha Musa, na chini ya uongozi wake Yoshua waliingia Kanani na kuwaua kwa upanga wenyeji wa nchi, na wakafanya maskani yao huko.

82. Je, Waisraeli waliishika sheria aliyowapa Mungu?

Jibu: Ni kwa muda mfupi tu. Halafu wakaasi sheria, na Mungu akawaadhibu kwa kuwaachilia watu wa mataifa mengine kuwashambulia, hatimaye, walitekwa na kutawanywa kama walivyo sasa katika nchi zote.

83. Je, kuna Waisraeli fulani kati ya hawa waliotawanywa katika nchi yetu?

Jibu: Ndio. Wanaitwa Wayahudi. Hakuna mtu anayewapenda wayahudi isipokuwa yule ampendaye Mungu. Mtu au watu wawapendao Wayahudi wanafanya hivyo kwa sababu ya Mungu.

84. Kwa nini wanaitwa Wayahudi?

Jibu: Walilipata jina hili ufalme wao ulipogawinyika. Sehemu moja ilikuwa ya makabila kumi waliokuja angamia baadaye, na sehemu nyingi ilikuwa haswa ya kabila la Yuda, na sehemu hii iliendelea kuwepo kwa muda wa kama miaka 800 baadaye. Kutoka kwa jina hili Yuda walipata neno Yu-s, yaani "Jews" (latamkwa "Jius").

85. Wayahudi watabakia katika hali hiyo ya kutawanywa milele?

Jibu: La. Mungu atawakusanya tena katika nchi yao Yesu atakaporudi mara ya pili. Na awafanye taifa lenye baraka wakiwa na Ibrahimu, Isaka na Yakobo, na watu wengine wote kati yao.

86. Wana wa Israeli walitawanywa kabla ya kuzaliwa kwake Yesu Bethlehemu?

Jibu: Ndio. Miaka sabini hivi kabla ya kuzaliwa kwake.

87. Yesu alikuwa na umri wa miaka mingapi alipojitokeza kwa taifa la Kiyahudi?

Jibu: Kama miaka thelathini.

88. Ni kitu gani alichofanya kati yao?

Jibu: Alizunguka kati yao akihubiri habari njema ya ufalme na kuponya magonjwa na kuwafufua wafu.

89. Alichukua muda gani kufanya haya?

Jibu: Miaka mitatu unusu.

90. Wayahudi walimfanyaje mwisho wa miaka hiyo?

Jibu: Walimwua kwa kumpigilia misumari kwenye mti.

91. Walimwua kwa nini?

Jibu: Kwa sababu wakuu wa watu hawakupenda kutolewa kwao makosa na Yesu.

92. Kwa nini Mungu aliwaachilia wamwue?

Jibu: Kwa sababu Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu ili Mungu apate kutusamehe na kutukubali kupitia kwa Yesu Kristo.

93. Mungu alimwacha Yesu kati ya wafu?

Jibu: La. Mungu alimfufua kutoka kwa wafu baada ya siku tatu.

94. Alienda wapi baada ya kutoka kaburini?

Jibu: Alikaa katika nchi takatifu hiyo muda wa zaidi ya majuma sita, akionana na wanafunzi wake mara kwa mara, na mwisho wa muda huo Mungu alimchukua mbinguni mahali alipo mpaka wa leo.

95. Kristo anafanya kazi gani sasa?

Jibu: Yeye sasa ni kuhani mkuu akifanya upatanishi kati yetu na Mungu, wale ambao wameliamini neno lake na kuchukua jina lake.

96. Wanaoamini wanachukuaje jina la Kristo?

Jibu: Kwa kuzikwa majini.

97. Kristo atabakia milele alipo sasa?

Jibu: La Yuaja tena duniani, kuwafufua wafu, na kuimarisha ufalme wake mtukufu katika nchi ya ahadi, na awaletee watu wote baraka ulimwenguni.

98. Zitakuwa siku za furaha wakati wa utawala wa Kristo?

Jibu: Zitakuwa siku za furaha kweli kweli. Kristo atatawala, ndugu zake watakuwa wafalme na makuhani wasiokufa, watu wote watakuwa na furaha na shida zote zitatokomea mbali. Kila mtu atakuwa na la kufanya na kufurahi ufalme wa Mungu. Hatimaye mauti yataondolewa, na laana haitakuwepo tena, uchungu na majonzi yatasahaulika.

99. Watakiwa ufanye nini ili uwe na nafasi kati ya watu hawa waliobarikiwa?

Jibu: Napaswa kufanya kama Mungu atakavyo.

100. Mungu akutaka ufanye nini?

Jibu: Kuamini Ukweli, nipate ubatizo kwa ondoleo la dhambi zangu, kuumega mkate kila siku ya kwanza ya wiki kama tulivyoagizwa, kuomba na kusoma Biblia kila siku; kumshukuru Mungu kwa kila jambo, kusema ukweli kila mara, kuwatendea mema wote kwa huruma, hata wale wasionipenda, tusitende maovu kwa wale watutendeao maovu, tukisemwa kwa ukali nasi tusitoe ukali, tuwe wangwana na wenye huruma, tuwe waaminifu, tuwe wavumilivu na watu watuone hivyo, tuwe wenye hekima na wenye kusamehe, kuwatendea watu yale ninayopenda wanitendee mimi, tusifanye urafiki na watu wabaya, lakini tushirikiane na watu wema katika kutenda mapenzi ya Kristo, na kungojea kuja kwake tena ili aimarishe ufalme wake mtukufu.


back