Amri za Kristo

Back

Amri za Kristo ni sehemu muhimu sana katika Ushirika wetu. Tusipojaribu kuziweka katika mawazo yetu, na kuzifuata, hatuna sehemu katika Mwili wa Kristo. " Matendo " ya " imani " yetu yanadhihirishwa kama ni hai au yamekufa. Hebu natuyatafakari kila mara, na yawe msingi wa matendo yetu yote.

1. Wapende adui zako; watendee mema wakuchukiao.

" ... lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi;... " (Mathayo 5:44).

2. Usiwapinge waovu: mtu akikupiga shavu la kushoto, mpe na la kulia.

" ...lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia " (Mathayo 5:39, 40).

3. Usilipize kisasi: epukana na hasira: kubali kupata hasara.

" Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana, imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana " (Warumi 12:18, 19).

4. Mtu akichukua mali yako, usiulize urudishiwe.

" Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang' anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu. Mpe kila akuombaye, na akunyang' anyaye vitu vyako, usitake akurudishie " (Luka 6:29, 30).

5. Patana na adui wako upesi, hata kukubali makosa kwa ajili ya amani.

" Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani " (Mathayo 5:25).

" Basi imekuwa upungufu kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyang' anywa mali zenu " (1 Wakorintho 6:7).

6. Usisumbukie utajiri: kuwa tayari kutenda mema, wape wakuulizao: wasaidie wahitaji

" ...ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo " (1 Timotheo 6:8).

" ...kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni, mkijitahidi "

(Warumi 12:13).

" Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu " (Waebrania 13:16).

" Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka " (Yakobo 1:17).

7. Usitoe ili kuonekana na watu: mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wa kuume.

" Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi " (Mathayo 6:1-4).

8. Usimlipe mtu maovu kwa maovu: shinda maovu kwa kutenda mema.

" Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote " (Warumi 12:17).

9. Wabariki wanaokulaani; laana isitoke kinywani mwako.

" ...lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi; " (Mathayo 5:44).

" Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani "

(Warumi 12:14).

10. Usilipe maovu kwa maovu, au matusi kwa matusi, bali ubariki tu.

" ...watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka "

(1 Petro 3:9).

11. Waombee hao wanaokudharau na kukutesa.

" ...lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi; " (Mathayo 5:44).

12. Usiwe na chuki, usihukumu, usinung'unike, usiwakatie wengine kesi.

" Ndugu, msinung'unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango " (Yakobo 5:9). " Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi " (Mathayo 7:1).

13. Tupilia mbali hasira, gadhabu, uchungu, na kila usemi wa uovu.

" Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; " (Waefeso 4:31).

" Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote "

(1 Petro 2:1).

14. Chukulianeni shida zenu.

" Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii " (Yakobo 5:16).

15. Usishiriki ya dunia: usipende mambo ya ulimwengu.

" Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu " (Warumi 12:2).

" Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake " (1 Yohana 2:15).

16. Katalia mbali mambo yasiyo ya Mungu na tamaa za ulimwengu. Mkono unaokusumbua, ukate.

" ...nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; " (Tito 2:12).

" Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee, wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum " (Mathayo 5:30).

17. Watumishi, iweni waaminifu hata kwa mabwana wabaya.

" Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo; wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekezao kwa wanadamu; bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo; kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu; mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana, kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru " (Waefeso 6:5-8).

18. Usiyafikirie mambo ya juu, bali toshekeni na mambo ya watu yakhe.

" Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili " (Warumi 12:16).

19. Usiwe na deni la mtu awaye yote.

" Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima. Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria " (Warumi 13:7, 8).

20. Kukitokea dhambi (inayojulikana au kushikika), usiwambie wengine, bali mwambie ndugu aliyekosa juu ya jambo hilo kati yako naye peke yenu, kusudi ni kurekebisha.

" Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo " (Mathayo 18:15).

" Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe " (Wagalatia 6:1).

21. Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote.

" Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote " (Mathayo 22:37).

22. Omba kila mara; omba kwa ufupi bila mambo mengi; omba kwa siri.

" Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa "

(Luka 18:1).

" Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi "

(Mathayo 6:7).

23. Katika kila jambo, mshukuru Mungu na umtambue katika njia zako zote.

" ...na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo; " (Waefeso 5:20).

" Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako "

(Mithali 3:6).

24. Jinsi mnavyotaka watu wawatendeeni ninyi, nanyi watendee vile vile.

" Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii "

(Mathayo 7:12).

25. Chukua mfano wa Kristo na ufuate nyayo zake.

" Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake " (1 Petro 2:21).

26. Kristo na adumu mioyoni mwenu kwa imani.

" Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; " (Waefeso 3:17).

27. Kristo na awe zaidi ya vitu vyote unavyovitaka duniani: naam, zaidi ya uhai wako.

" Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu " (Luka 14:26).

28. Mkiri Kristo waziwazi mbele ya watu.

" Nami nawaambia, kila atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri yeye mbele ya malaika wa Mungu; " (Luka 12:8).

29. Jihadhari, mahitaji ya maisha na mvuto wa anasa usilegeze upendo wake kwako wewe.

" Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo; kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima. Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika hayo yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu " (Luka 21:34-36).

30. Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe.

" Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako " (Mathayo 22:39).

31. Usiwe bwana mkubwa juu ya ye yote.

" Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo. Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa " (Mathayo 23:10-12).

32. Usijifikirie kibinafsi, wala kujitatulia matatizo yako tu, bali waangalie na wengine.

" Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine " (Wafilipi 2:4).

" Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo "

(Wagalatia 6:2).

33. Nuru yako na iangaze mbele ya watu: lishike vema Neno la Uzima. Watendee watu wote mema ukiwa na nafasi.

" Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni " (Mathayo 5:16). " ...mkishika neno la uzima; nipate sababu ya kuona fahari katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio bure wala sikujitaabisha bure " (Wafilipi 2:16).

" Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio " (Wagalatia 6:10).

34. Ishi bila lawama na usimdhuru mtu, kama wana wa Mungu katikati ya kizazi kiovu na kilichopotoka.

" ...mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu... " (Wafilipi 2:15).

35. Uwe mngwana, mpole, mwenye moyo safi, rehema, huruma, mwenye kusamehe.

" Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu... " (2 Timotheo 2:24).

" ...ya kwamba wazee wawe wenye kiasi, wastahivu, wenye busara, wazima katika imani na katika upendo na katika saburi " (Tito 2:2).

" ...tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi "

(Waefeso 4:32).

36. Uwe na kiasi, usichukulie mambo hivi hivi, uaminike, uwe kadiri.

" Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu " (Wafilipi 4:5). " Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo " (1 Petro 1:13).

" Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze "

(1 Petro 5:8).

37. Semeni ukweli kila mtu na jirani wake: epukana na uongo wa kila namna.

" Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake " (Waefeso 4:25).

38. Cho chote mfanyacho, kifanye kama kwamba wamfanyia Bwana, wala sio wanadamu.

" Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, " (Wakolosai 3:23).

39. Kesha, uwe macho, jasiri, mwenye furaha, adabu njema na tenda kiume.

" Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari " (1 Wakorintho 16:13).

" Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini "

(Wafilipi 4:4). " Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi. Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku. Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu. Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo; ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, kwamba twakesha au kwamba twalala " (1 Wathesalonike 5:6-10).

40. Jivike upole: uwe na saburi kwa watu wote.

" Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,... " (Wakolosai 3:12).

" ...kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu;... "

(Warumi 12:12).

41. Ishi kwa amani na watu wote.

" Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;... " (Waebrania 12:14).

42. Shiriki furaha na huzuni ya wengine.

" Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao " (Warumi 12:15).

43. Yafuate yote yaliyo ya kweli, haki, safi, kupendeza, sifa nzuri, wema, na kusifika.

" Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo " (Wafilipi 4:8).

44. Jiepushe kabisa na uzinzi, uasherati, uchafu, ulevi, tamaa, ghadhabu, mashindano, uasi, chuki, uigaji, kujidai, kujipendekeza, wivu, mzaha na maongezi ya upuzi.

" Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wala kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru " (Waefeso 5:3, 4).

45. Lo lote utendalo, fikiria matokeo yake katika kulitukuza Jina la Mungu kati ya watu. Yote yafanyike kwa utukufu wa Mungu.

" Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu " (1 Wakorintho 10:31).

" Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi "

(1 Wakorintho 3:17).

46. Jihesabuni wafu kwa dhambi ya kila namna. Tangu sasa ishini kwa sababu ya yule aliyekufa kwa ajili yenu na kufufuka tena.

" Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi, na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu " (Warumi 6:11).

" ...tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao "

(2 Wakorintho 5:15).

47. Usichoke katika kutenda mema, ukitenda kazi ya Bwana.

" ...ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema " (Tito 2:14).

" Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho "

(Wagalatia 6:9).

48. Usiseme maovu juu ya mtu awaye yote.

" ...wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote " (Tito 3:2).

49. Neno la Kristo na likae ndani yenu.

" Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu " (Wakolosai 3:16).

50. Uneni wenu uwe wa kupendeza, utiliwe chumvi kiasi.

" Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu "

(Wakolokai 3:8).

" Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu "

(Wakolosai 4:6).

51. Tii watawala; tii kila mamlaka kwa ajili ya Bwana.

" Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema;... " (Tito 3:1).

52. Mazungumzo yako yote yawe ya kupendeza.

" ...bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu " (1 Petro 1:15, 16).

53. Usimpe adui nafasi kusema mabaya juu yako.

" Basi napenda wajane, ambao si wazee, waolewe, wazae watoto, watawale na madaraka ya nyumbani; ili wasimpe adui nafasi ya kulaumu " (1 Timotheo 5:14).


Back